Habari za Punde

ZIRPP Monthly Lecture: "Muswada kuhusu Mafuta na Gesi Asilia ya Zanzibar na Umiliki wa Kisiwa cha Fungu Mbaraka (Latham Island)"

Chairperson: Mr. Muhammad Yussuf


Speaker: Mr. Othman Masoud Othman Sharif
Subject: "Muswada kuhusu Mafuta na Gesi Asilia ya Zanzibar na Umiliki wa Kisiwa cha Fungu Mbaraka (Latham Island)"
Date & Time: Saturday 29 October 2016; at 4:00 pm.
Venue: ZIRPP Office,Third Floor, behind Majestic Cinema (above ZANLINK
 
ABSTRACT: Hivi karibuni, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Mheshimiwa Zitto Kabwe, amewasilisha rasmi Muswada binafsi wa Sheria ya Mabadiliko ya 15 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Mafuta na Gesi Asilia ya Zanzibar. Zitto amesema amefanya hivyo ili kuhalalisha hatua ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya kutunga Sheria inayohusiana na suala la Mafuta na Gesi Asilia ambayo imepitishwa hivi karibuni na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
 
Hata hivyo, hoja ya Baraza la Wawakilishi kuidhinishwa na Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kutunga Sheria ya Mafuta ya Zanzibar, imezua masuala mengi zaidi kuliko majibu. Miongoni mwa masuala hayo ni kwamba, kwa mujibu wa Kanuni ya Kutunga Sheria (legislative principles), Sheria haiwezi kukasimu mamlaka ya kutunga Sheria nyengine. Sheria siku zote inakasimu uwezo wa kutunga kanuni; yaani Sheria ya kukasimiwa (delegated legislation).
 
Kwa hivyo, kwa kuruhusiwa na Bunge, vipi Baraza litatunga Sheria badala ya kuwa limetunga Kanuni tu?  Hata kama Sheria hiyo iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi itaitwa Sheria lakini msingi wa nasaba yake hauipi hadhi ya kuwa Sheria.   Aidha, katika hoja hii ya Baraza la Wawakilishi kuidhinishwa na Bunge ipo hoja kwamba Sheria hiyo ya Baraza la Wawakilishi inagongana na Sheria ya Bunge ambayo inadaiwa kutoa idhini.  Wakati Sheria hiyo ya Bunge imetoa uwezo kwa Zanzibar kutunga Sheria ya kuunda vyombo vya kusimamia Sheria hiyo ya Bunge kwa upande wa Zanzibar, Baraza la Wawakilishi limetunga Sheria ya jumla ya Mafuta sawa na ile Sheria ya Bunge.  Kwa hivyo, Sheria hizo mbili zina mgongano wa wazi ambao unafanya utekelezaji wake kisheria usiwezekane.
 
Hoja hiyo ya kutungwa kwa Sheria ya Mafuta ya Zanzibar, pia iliambatana na ile ya masharti ya Ibara ya 64 ya Katiba ya JMT inayosema kuwa endapo Baraza la Wawakilishi litatunga Sheria kwa jambo ambalo limo mikononi mwa Bunge, Sheria hiyo itatenguka kwa kuwa itakuwa ni batili. Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamediriki kudai kuwa Baraza limepitisha Sheria hiyo ili wapate nguvu ya kudai mipaka ya nchi ya Zanzibar; kwani mipaka ni katika mambo madogo madogo ya kushughulikiwa baadaye. Kwa mfano, kisiwa cha Fungu Mbaraka (Latham) ambacho ni sehemu ya Zanzibar, tayari kimeshavamiwa na Serikali ya Tanzania Bara na  kutangazwa rasmi katika makongamano ya kimataifa, kama vile lile lililofanyika Chatham House tarehe 26 Februari 2013.
 
Kwa ujumla suala la kutungwa kwa Sheria ya Mafuta na Baraza la Wawakilishi ambalo lilipaswa liwe la manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa Zanzibar na liwe ni jambo ambalo litaweza kutatua moja ya kero za wazi za Muungano, badala yake imeleta kitendawili kipya, utatanishi mkubwa na kuimarisha kero hii ya muda mrefu ya Muungano.
 
Katika kulijadili kwa kina, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, Othman Masoud Othman, atapata fursa ya kulielezea suala hili kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizopo na jinsi ambavyo suala la Mafuta na Gesi Asilia linavyohusiana na haki na mamlaka ya Zanzibar katika kulishughulikia kwake kwa faida na maslahi ya Zanzibar na watu wake, ikiwa ni pamoja na athari ya kutotatuliwa suala la mipaka baina ya Tanzania Bara na Zanzibar katika suala la utafutaji na uchimbaji wa rasilimali ya Mafuta na Gesi Asilia.  Mfano mzuri wa utatanishi wa mipaka ni suala la umiliki wa kisiwa cha Fungu Mbaraka (Latham) ambacho ni mali halisi ya Zanzibar tokea mwaka 1898 na kimeendelea hivyo hata baada ya uhuru wa Zanzibar mnamo mwaka 1963 na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
 
Tea, Coffee and Snacks will be served freely.
 
Please forward this message to anybody who may be interested. Those who would like to attend should send their email addresses and telephone numbers to: zirpp@googlegroups.com.
 
Please confirm your participation. You may bring one or two friends with you.
 
All are welcome.
 
 
Muhammad Yussuf
Executive Director
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 4523, Zanzibar, Tanzania;
Tel: +255 242 223-8474;
Fax: +255 242 223-8475;
Cellular: 0777 707820;
Website: www.zirpp.info
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.