Habari za Punde

Mama Mwanamwema Shein Aendelea na Ziara yake Kisiwani Pemba Kuzungumza na Wanawake UWT Kutoa Shukrani.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Wilaya Mkanyageni Mkoani Pemba kuzungumza na Wanawake hao kutowa shukrani kwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliopita.
Viongozi wa UWT Wilaya ya Mkoni Pemba wakimkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, alipowasili katika ukumbi wa majengo ya Skuli ya Sekondari ya Mkanyageni Mkoani Pemba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisaini kitabu cha wageni alipowaili katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya katika Kijiji cha Mkanyageni Mkoani Pemba.
Kiongozi wa UWT Wilaya ya Mkoani Pemba Bi Naima Nahodha akisoma Quran kabla ya kuaza kwa mkutano wao na Mke wa Rais wa Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya ya Mkoani. 
Katibu wa UWT Wilaya ya Mkoani Pemba Bi Amina Haji akitowa maelezo machachi wakati wa mkutano wao na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kutowa shukrani kwa Wananchi wa Wilaya ya Mkoani.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, akizungumza wakati wa mkutano huo na kutowa nasaha zake kwa Viongozi wa UWT Wilaya ya Mkoani wakati wa Mkutano na Mke wa Rais wa Zanzibar Mamas Mwanamwema Shein,kutowa shkrani kwa wananchi hao.   
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume, akizungumza wakati wa mkutano huo na kutowa nasaha zake kwa Wanawake wa Wilaya ya Mkoani na kutowa historia ya Wanawake katika Zanzibar, wakati wa mkutano wa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kutowa shukrani kwa Wananchi hao.  
Baadhi ya Viongozi wa UWT wa Wilaya ya Mkoani Pemba wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya Mkanyageni Pemba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Kadi ya Uwanachama  mwanachama mpya wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Mkoani Pemba Bi. Biubwa Ridhiwani,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya Mkanyageni Pemba wakati wa mkutano wake na Viongozi wa UWT wa Wilaya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya Mkanyageni Pemba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Kadi ya Uwanachama  mwanachama mpya wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Mkoani Pemba Bi. Maryam Ali,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya Mkanyageni Pemba wakati wa mkutano wake na Viongozi wa UWT wa Wilaya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya Mkanyageni Pemba.Jumla ya Wanachama wapya wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania 30 wamejiunga na kukabidhiwa Kadi.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.