Habari za Punde

Kikosi Kazi cha Watu Kumi Kitakachoshambulia Kongamano la Sauti ya mwanamke Jijini Mwanza leo.

Leo linafanyika Kongamano kubwa la Sauti ya Mwanamke Jijini Mwanza kuanzia saa kumi alasiri ndani ya Gold Crest Hotel. Kongamano limeandaliwa na kampuni ya Chocolate Princes inayoandaa kipindi cha The Mboni Show cha Mboni Masimba.

Kuna elimu, burudani, chakula na vinywaji kwa elfu arobaini tu hivyo usithubutu kukosa kwani kikosi cha zaidi ya watu kumi tayari kimejipanga sawa sawa kufanya kazi yake ipasavyo.

Tayari tiketi za kongamano hilo litakalofanyika tarehe sita mwezi huu kwenye ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza zimeanza kuuzwa kwa shilingi elfu arobaini katika maeneo mbalimbali ikiwemo Gold Crest Hotel, TSN Super Market Rock City Mall, Flora Salon, Kayvies Beaty Parlour Magnum Hotel Ghana, Idda Garments, Diamond Bar Kona ya Bwiru pamoja Bladict Classic Wear mtaa wa Uhuru Dampo.
Na BMG Habari
Bonyeza HAPA Kwa Taarifa Zaidi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.