Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akimfariji Mke wa Spika Mstaafu wa Tanzania Mzee Samuel Sita, Mama Magret Sita walipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere Jijini Dar es salaam na mwili wa Marehemu ukitokea Nchini Ujerumani alikofariki Dunia wakati akipatiwa matibabu.
Mheshimiwa Samia akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiendelea kumfariji Mama Magret Sita kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam wakati wa mapokezi ya kitaifa ya mwili wa Marehe Mzee Samuel Sita.
Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania wakiuteremsha mwili wa Spika Mstaafu wa Tanzania Marehemu Samuel Sita kwenye gari maalum la kubebea maiti la Jeshi la wananchi wa Tanzania kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere.
Askari wa jeshi la Polisi Tanzania wakiubeba mwili wa aliyekuwa Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania Mzee Samuel Sitaukitokea Ujerumani alikokuwa akipata matibabu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitia saini Kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Spika Mstaafu waBunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Marehemu Samuel Sita Nyumbani kwake Mtaa wa Masaki Jijini Dar es salaam.
Pembeni kushoto ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na mbele yake Balozi ni Picha ya Marehemu Mzee Samuel Sita.
Kikundi maalum cha Kwaya kilichotayarisha maalum kuimba nyimbo za maombolezo Nyumbani kwa Marehemui Mzee Samuel Sita wakati ibada za kuuaga mwili wake zikiendelea kwa Viongozi wa Kitaifa, Marafiki pamoja na wana Familia nyumbani kwake Masaki Mjini Dar es salaam.
Baadhi ya wageni na wana familia waliohudhuria misa maalum ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ambae pia ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Samuel Sita.
Picha na – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment