Habari za Punde

Naibu Waziri wa Habari , Utalii, Utamaduni na Michezo azungumza na Masheha wilaya ya Micheweni

 Naibu Waziri wa Habari , Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bichumu Kombo Khamis, akizungumza na Masheha wa Wilaya ya Micheweni Pemba, juu ya kulinda na kuimarisha vivutio vya Utalii ambavyo ni vyanzo vya ukuzaji wa mapato kupitia sekta hiyo.
 Ofisa Mdhamini Wizara ya Habari , Utalii , Utamaduni na Michezo Pemba, Khatib Juma Mjaja, akitowa maelezo kwa masheha juu ya umuhimu wa utunzaji wa vivutio vya Utalii yakiwemo magofu , mapango n,k yalioko katika eneo Wilaya hiyo na kuyapatia hati miliki ili kuepusha kuvamiwa na watu wengine kwa shuhuli zao binafsi.


Baadhi ya masheha wa Wilaya ya Micheweni Pemba, wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Habari, Utalii , Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bichumu Kombo Khamis, wakati alipokuwa akizungumza nao juu ya kuimarisha na kulinda vivutio vya Utalii Wilayani humo.

Picha na Hanifa Salim -Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.