Habari za Punde

NUHU AMSOGEZA BUI AFRIKA YA KUSINI

Beki wa kushoto wa klabu ya Mafunzo Samih Haji Nuhu ambaye ametimkia Afrika ya Kusini kujaribu zari la kutafuta timu ya kuchezea amemuita mchezaji mwenzake anayecheza nafasi ya kiungo


Taarifa za uhakika kutoka ndani ya klabu ya Mafunzo zilithibitisha juu ya kuondoka kwa kiungo huyo mshambuliaji ambaye ameiwacha timu yake ikiwa bado inaendelea ya mchakato wa ligi kuu visiwani Zanzibar.

Nuhu amemuita Abdulaziz Makame maarufu Bui mara nyingi hucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji kutokea upande wa kushoto.

Akithibitisha kuhusiana na taarifa hii katibu wa klabu ya Mafunzo Makame Fadau alisema Abdulaziz Makame aliondoka baada ya kufanyiwa mpango na mchezaji mwenzake.

"Ni kweli Bui kwa sasa hayupo kwenye kikosi chetu ameelekea Afrika ya Kusini kufanya majaribio"

Hata hivyo Fadau hakutaka kuitaja timu ambayo mchezaji huyo ameelekea kwa madai ya kuwa bado mchakato unaendelea huku akiahidi endapo dili litakaa sawa basi wataitangaza timu hiyo.

Mchezaji huyo ambaye kwa umbo amepanda juu aliwahi pia kuichezea timu ya Simba ya jijini Dar es salaam kabla ya kurejea Mafunzo kwenye dirisha dogo la usajili mwaka jana.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.