Habari za Punde

TANZIA: Familia ya Binagi Iliopo Jijini Dar es Salaam Inasikitika Kutangaza Kifo cha Mzee Wao, Richard Binagi.

Familia ya Binagi iliyopo Kipunguni Jijini Dar es salaam, inasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao, Mzee Richard Maihagya Binagi, kilichotokea leo Novemba 08,2016 asubuhi, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Habari ziwafikie wanafamilia wote wa Binagi waliopo mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dar es salaam, Mwanza na Mara pamoja na watoto wa marehemu walio nje ya nchi ikiwemo Marekani, bila kuwasahau ndugu, jamaa na marafiki.

Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Jijini Dar es salaam. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake Libarikiwe, Amina!

Kumbukumbu: Marehemu Mzee Richard Maihagya Binagi alizaliwa mwaka 1928 Tarime mkoani Mara hivyo hadi mauti yanamkuta (2016), alikuwa na miaka 88 ambapo alikuwa ni askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.