Habari za Punde

Maziko ya aliyekuwa Mwenyekiti wa kamisheni ya Utalii Zanzibar Marehemu Saleh Ramadhan Feruzi

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji na kumpa pole mke wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar ambe pia ni Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar Nd. Saleh Ramadhan Ferouz aliyefariki dunia jumatatu kutokana na maradhi ya Saratani ya  Tezi dume.

 Waumini wa dini ya Kiislamu wakiambatana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Rais wa Serikali ya Muungano Dr. Moh’d Gharib Bilal pamoja na Viongozi wengine wa Kisiasa na Serikali wakimsalia Marehemu Saleh Ramadhan Ferouz katika Msikiti wa Ijumaa wa Kiembe Samaki.
 Balozi Seif akitia mchanga katika kaburi la aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Maheremu Ferouz aliyezikwa katika Makaburi ya Mwanakwerekwe nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Moh’d Gharib Bilal akitia mchanga katika Kaburi la marehemu Saleh Ramadhan Ferouz hapo Mwanakwerekwe.


Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitia mchanga katika Kaburi la mtangulizi wake katika nafasi hiyo ya Chama Marehemu Saleh Ramadhan Ferouz KATIKA Makaburi ya Mwanakwerekwe.

Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.