Habari za Punde

Uzinduzi wa Hospitali Mpya ya Abdallah Mzee Pemba leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (katikati) na Mkurugenzi  wa huduma za Hospitali Mohamed Dahoma na Viongozi wengine wakiwa katika chumba cha uchunguzi wa matatizo ya uti wa mgongo  baada ya kuizindua rasmi Hospitali ya Abdalla Mzee  iliyopo  Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt.Juma Malik Akil wakifuatana na Viongozi wengine wakati alipotembelea Hospitali ya Abdalla Mzee  iliyopo  Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kuizindua rasmi leo (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe, Mwanajuma Majid  hospitali hii imejengwa na  Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kutembelea sehemu mbali mbali za Hospitali ya Abdalla Mzee  iliyopo  Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kuizindua rasmi leo (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe, Mwanajuma Majid  hospitali hii imejengwa na  Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar dk Juma Malik Akil, akizungumza kwenye ufunguzi wa jengo jipya la hospitali ya Mkoa ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, ambalo limejengwa upya, na baadhi ya majengo yake kufanyiwa ukarabati mkubwa, na serikali ya amhuri ya watu wa China, ambayo imefunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein
 Balozi wa China nchini Tanzania, Lv You Qing  akieleza namna ya ushirikiano ulivyo baina ya nchi yake na Tanzania –kwenye ufunguzi wa jengo jipya la Hospitali ya Mkoa ya Abdall Mzee Mkoani Pemba, ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na baadhi ya majengo kujengwa upya na serikali ya watu wa China
 Waziri wa Afya Zanzibar Mahamuod Thabiti Kombo, akizungumza kwenye ufunguzi wa jengo jipya na la kisasa la hospitali ya Mkoa ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, ambayo, imejengwa na kufanyiwa ukarabati mkubwa na serikali ya watu wa China
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Afisa Mdhamini wa wizara ya Afya Pemba, Bakar Ali Bakar picha maalumu ya muasisi wa Hospitali ya Abdalla  Mzee, bwana Abdalla Mzee, kwenye hafla ya kuifungau hospitali hiyo, ambayo imejengwa na kufanyiwa matengenezo makubwa na na serikali ya watu wa China
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi maalum Balozi wa Chini nchini Tanzania Lv You Qing kutambua mchango wao, katika sekta ya afya, hafla  hiyo ilifanyika kwenye ufunguzi wa hospitali ya Mkoa wa Abdalla Mzee Mkoani Pemba, ambayo imejengwa na kufanyiwa matengenezo makubwa na na serikali ya watu wa China


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na mamia ya wananchi wa Pemba, baada ya kulifungua jengo jipya na la kisasa la hospital ya Mkoa ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, baada ya kujengwa upya na kufanyiwa matengenezo makubwa na serikali ya watu wa China.
, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.