Habari za Punde

Kampuni ya Simu ya Zantel Yamwaga Vifaa kwa Wakulima wa Mwani Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasi Mifugo na Uvuvi Ndg Ali Juma Ali akimkabidhi vifaa vya Upandaji wa Mwani Bi. Timamu Yussuf, Mwnyekiti wa Kikundi cha Wakulima wa Mwani Jambiani Kibigija Wilaya ya Kusini Unguja, Vifaa hivyo vya kilimo cha Mwani vimetolewa na Kampuni ya Simu ya Zantel, Jumla ya Vikundi vya kilimo cha mwani Zanzibar 48 vimekabidhi kamba na Taitai kwa ajili ya kupandia zao hilo, katikati Afisa Masoko wa Zantel Zanzibar Ndg Haji Khatib na kulia Mkurugenzi wa Uvuvi Zanzibar Ndg Mussa Aboud Jumbe . Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Wizara ya Kilimo Maruhubi Zanzibar
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasi Mifugo na Uvuvi Ndg Ali Juma Ali akimkabidhi vifaa vya Upandaji wa Mwani Bi. Timamu Yussuf, Mwnyekiti wa Kikundi cha Wakulima wa Mwani Jambiani Kibigija Wilaya ya Kusini Unguja, Vifaa hivyo vya kilimo cha Mwani vimetolewa na Kampuni ya Simu ya Zantel, Jumla ya Vikundi vya kilimo cha mwani Zanzibar 48 vimekabidhi kamba na Taitai kwa ajili ya kupandia zao hilo, katikati Afisa Masoko wa Zantel Zanzibar Ndg Haji Khatib na kulia Mkurugenzi wa Uvuvi Zanzibar Ndg Mussa Aboud Jumbe . Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Wizara ya Kilimo Maruhubi Zanzibar, mwenye sati nyeupi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Dk Islam Seif.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasi Mifugo na Uvuvi Ndg Ali Juma Ali akitowa shukrani kwa Afisa wa Masoko wa Kampuni ya Zantel Zanzibar Ndg Haji Khatib, baada ya hafla hiyo ya kukabidhi Vifaa hivyo kwa Wakulima wa Mwani Zanzibar Hafla iliofanyika katika viwanja vya Wizara ya Kilimo Maruhubi Zanzibar. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Ndg Juma Ali Juma akizungumza na Viongozi wa Vikundi vya Wakulima wa Mwani Zanzibar katika ukumbi wa Wizara hiyo ulioko maruhubi Zanzibar.  


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.