Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein Mgeni Rasmin Maulidi ya Kuzaliwa Mtume (S.A.W) Viwanja vya Maisara Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Sheikh Sherali Champsi mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Baadhi ya Viongozi na waalikwa mbali mbali wakiwa katika Sherehe ya kuadhimisha Maulid ya kuzalia Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
Mke wa Rais wa Zanzibar  Mama Mwanamwema Shein(katikati) akiwa na wake wa Viongozi mbali mbali na Wananchi wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya Maulid ya kuzalia Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akimkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) katika  Maulid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akimuangalia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akitia ubani kama ishara ya Kuyafungua Maluid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Waislamu na Wananchi waliohudhuria katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Ustadh Ali Muombwa Hassan wa Chuo cha Kiislamu akitoa Tafsiri ya Qur'aan Tukufu  ya Suratul Touba (Aya 128 hadi 129) iliyosomwa  katika  sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Wanafunzi wa Madressa Hidayatul Munineema na Nurul Islamia ya Mpendae Mjini Unguja wakisoma Qaswida YaRabii Swali katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Ustadh Mohamed Khamis Rashid wa Kiweani Pemba akisoma maulid Barzanji mlango wa kwanza katika sherehe tukufu ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akifukiziwa Udi baada bya kutiliwa marashi wakati kumswalia mtume Muhamad (S.A.W) wakati sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa kiongozi huyo   sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Wake wa Viongozi wakisimama kumswalia Mtume (S.A.W) wakati wa Maulid ya Maadhimishio yas Sherehe ya Kuzaliwa Kiongozi wetu wa Dini ya Kiislamu zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja 
Mashekhe mbali mbali na wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya Maulidi ya kuzaliwa Kiongozi wetu Mtume Muhammad (S.A.W) wakisimama kumswalia jana katika sherehe zilizofanyika katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipookea Zawadi ya Qaswida ya mwaka kutoka kwa Sheikh Sherali Champsi, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) wakati wa sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja 
Sheikh Mohamed Kassim akitoa Khutba yake wakati wa  sherehe za maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)  sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja 
Wanamadrssa kutoka Mtendeni Mjini Unguja wakisoma Maulid ya Hom wakati wa sherehe za maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)  sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja 
Akina mama waliojitokeza katika sherehe za maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)  sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja 
Wanafunzi wa Madrassa  mbali mbali na Wananchi wakiwa katika sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)  sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na  Sheikh Sherali Champsi Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) baada ya kumalizika kwa sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,(kushoto) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud,[Picha na Ikulu.] 11/12/2016.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.