Habari za Punde

Wizara ya Ardhi Yapima Viwanja Zaidi ya Milioni Moja na Mashamba Elfu 24

Frank Mvungi. Maelezo Dar es Salaam.
6.12.2016
SERIKALI imefanikiwa kupima viwanja zaidi ya Milioni moja na mashamba takribani elfu ishirini na nne ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuhakikisha kuwa kila kipande cha Ardhi kinapimwa na kumilikishwa.
auli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Idara ya upimaji na ramani toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Bw. Justo Lyamuya wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

“Upimaji wa mashamba umekuwa ukipungua na ule wa Viwanja kuongezeka kutokana na maeneo mengi ya mashamba kugeuka kuwa maeneo ya mpango na hivyo kuandaliwa michoro na kupimwa viwanja” alisisitiza Lyamuya.

Akizungummzia suala la Vijiji Lyamuya amesema vijiji 10,667 kati ya vijiji 12,000 chini ya mradi wa land Tenure Support Programme vimepimwa.

Aliongeza kuwa upimaji ardhi chini ya maji katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo umefanyika kwa kushirikiana na jeshi la Maji la India wameweza kupima Bandari za Dar es salaam, Zanzibar , Mkoani Pemba ambapo ramani za Bandari hizo zipo tayari.

Anaongeza kuwa katika kipindi cha mwaka huu upimaji wa bandari ya Tanga umefanyika na kazi ya uwandani imekamilika na maandalizi ramani ya eneo hilo yanaendelea.

Akizungumzia changamoto zinazokabili sekta ya ardhi, Lyamuya alisema kuwa baadhi ya wapimaji wenye leseni wamekuwa wakisaini kazi za upimaji ambazo hawajazisimamia ambazo mara nyingi zimefanywa na “vishoka”  na kuziwasilisha kwa ajili ya uidhinishaji kinyume cha Sheria na taratibu zinavyotaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.