Habari za Punde

Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup Timu ya Taifa ya Jangombe Imefanikiwa Kuingia Nusu Fainali Baada ya Kuifunga URA Kwa Bao 1--0.


Mabingwa Watetezi wa Kombe la Mapinduzi Cup URA ,kutoka Nchini Uganda wakiwa na butwaa baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Timu ya Taifa ya Jangombe katika mchezo wao wa mwisho kuwania kucheza nusu fainali ya michuano hiyo ya 11 ya Mapinduzi Cup inayofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Timu ya Taifa ya Jangombe itaungana na Timu za Yanga, Simba na Azam katika mchezo wa Nusu Fainali utakaofanyika siku ya Jumanne katika uwanja wa Amaan Zanzibar. kwa mechi mbili jioni na usiku 

Katika mchezo wa jioni wa michuano hiyo hatua ya nusu fainali itazikutanisha Timu ya Taifa ya Jangombe na Azam  utachezwa kesho jioni na wakati wa usiku nyasi za uwanja wa Amaan  zitapata kishindo cha mchezo wa watani wawili Simba na Yanga zitaumana kuwania nafasi ya kucheza fainali tarehe 13-1-2017. kuhitimisha michuano hiyo ya kumi na moja ya Mapinduzi Cup,  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.