Habari za Punde

Mtoto afariki baada ya kuanguka katika ndoo ya maji

Na mwandishi wetu Pemba

Mtoto mmoja mwenye wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu Khadija Said Mbarouk mkaazi wa Kichunjuu shehia ya Mizingani wiliya ya mkoani mkoa wa kusini Pemba amefariki dunia baada ya kuzama katika ndoo iliyokua na maji. 

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12:45 maghribi mara baada ya mama mzazi wa mtoto huyo Fatma Hafidh alipokua akisali na baada ya kumaliza na kutoka nje ndipo alipomuona mtoto wake akiwa katika ndoo hiyo.

Akizungumza kwa majonzi baba mzazi wa mototo huyo Saidi Mbarouk amesema kua mara baada ya kutokea tukio hilo waliamua kumchukua mtoto na kumkimbiza katika hospitali ya Abdallah Mzee na ndipo walipopatiwa majibu kua ameshafariki dunia.

“kama tunavyojua sote ni wa mungu na hakika sote tutarejea kwake hii ni asababu tu na kila mmoja na wakati wake na ukifika hakuna ujanja tunamshukuru mungu kwa tukio hili” alisema bw Hafidh. 

Amesema kutokana na mkasa huo hawanabudi kumshukuru Mwenyezimungu kwakua kifo ni haki ya kila mtu na kilichotokezea ni sababu tu ya kifo chake.

Babu wa mtoto Bw Kassim Juma Abdallah amemuambia mwandishi wa habari hizi huku akionekana kua na simanzi kua inagawa wanaumia sana kutokana na tukio hilo lakini bado wamo katika subra wakiamini kua hiyo ni mipango ya Allah SW.

Kwa upande wake sheha wa shehia ya Mizingani Bw Rajab Mbwana Rajab amesema kua amelipokea tukio hilo kwa mshituko mkubwa huku akisema kua ni la kuhuzunisha hasa kwa wanafamilia hiyo kuondokewa na kipenzi chao.

Sheha huyo amewataka wafiwa kua na moyo wa subra kwani mauti ni haki ya kila mtu.

Sambamba na hayo amewataka wazazi na walezi wa watoto kuzidisha umakini katika malezi ya watoto kwa kujua mazingira wanayochezea watoto wao pamoja na kuweka pembeni au mbali vitu vyote vile vitakavyokua na muonekano wa kuweza kusababisha hatari kwa mtoto.

Kamanda wa polisi mkoa wa kusini Pemba Shekhani Muhammed Shehan amesema kua mpaka sasa hakuna taarifa ya tukio hilo iliyoripotiwa katika kituo cha polsi.

Amesema inaonekana wanafamilia hiyo hawakutoa taarifa katika kituo cha polsi.

Habri kutoka kwa wanafamilia ya mtoto huyo zinasema kua mtoto Khadija alifariki tokea nyumbani na waliamua kumpeleka hospitali ili kwenda kupata uthibitisho tu wa daktari. 

Wananchi kutokana maeneo mablimbali ya shehia ya Mizingani walikusanyika pamoja leo saa 1 za asubuhi kuuzika mwili wa mtoto huyo huko Kichinjuu,Innalalillahi wainnailyhirajiun.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.