Habari za Punde

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Yaandaa Kongamano na Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar Kujenga Ushirikiano na Waandishi.

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar(ZSSF) Mussa Yussuf akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kabla ya ufunguzi wa Kongamano hilo la kujenga ushirikiano baina ya pande hizo mbili, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Jengo la Malaria Mwanakwerekwe Zanzibar. 
Meneja Utawala na Rasilimali Watu wa Mfuko wa Jamii Zanzibar (ZSSF) Ndg. Makame Mwadini akifungua mkutano wa Kongamano  na Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Malaria Mwanakwerekwe Zanzibar kuzungumzia uendeshaji wa Mfuko huo kwa Jamii. 
Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar wakimsikiliza Meneja Utawala na Rasilimani Watu wa ZSSF akifungua Kongamano hilo la Wahariri wa Vyombo vya habari Zanzibar.
Meneja Huduma wa Mfuko wa Jamii Zanzibar ZSSF Ndg Khamis Fil-Fil Thani akitowa Mada kuhusu uendeshaji wa Mfuko wa ZSSF kwa Washiriki wa Kongamano hilo lililowakutanisha Wahariri na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali na Binafsi kuzungumzia ufanisi wa Mfuko huo, na kujenga mahusiano na Vyombo vya habari kutowa taarifa kwa wananchi juu ya mfoko wao.
Waandishi wa Habari na Wahariri wakifuatilia Mada wakati wa Kongamano hilo lililoandaliwa na Mfuko wa Jamii Zanzibar kutoa taarifa na kuufahamu mfuko huo lililofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Malaria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mwanasheria wa Mfuko wa Jamii Zanzibar ZSSF Ndg Mohammed Faki Mzee akitowa Mada ya Marekebisho ya Sheria ya Mfuko wa ZSSF wakati wa Kongamano hilo lililowakutanisha Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar vya Serikali na Binafsi lililofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Malaria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Waandishi na Wahariri wakifuatilia mada hiyo wakati ikiwasilishwa wakati wa Kongamano hilo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.