Habari za Punde

Timu ya Ferroviario De Beira ya Msumbuji Yawasili Zanzibar Tayari kwa Mchezo Wao wa Klabu Bingwa na Timu ya Zimamoto ya Zanzibar

Wachezaji wa Timu ya Ferroviario De Beira ya  kutoka Nchini Msumbuji ikiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza na Timu ya Zimamoto unaotarajiwa kufanyika tarehe 11-2-2017 katika Uwanja wa Amaan Zanzibar Mchezo huo utafanyika majira ya saa 10.00 jioni. 
 Na mchezo wa marudioano unatarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji.
Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar ikiwa na Wachezaji wa Timu ya Ferroviario De Beira ya Msumbiji. ikiwa na Wachezaji na Viongozi 26. 
Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Zanzibar ZFA , Mzee Zam, .mwenye shati la mistari akiwa na viongozi wa Timu ya Ferroviario De Beira ya Msumbiji wakati alipofika kuipokea Timu hiyo kwa ajili ya Mchezo wake wa Klabu Bingwa  na Timu ya Zimamoto ya Zanzibar mchezo unaotarajiwa kufanyika siku ya terehe 11-2-2017 katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Wachezaji wa Timu ya kutoka Msumbiji wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo mchana na Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia 










No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.