Eneo la Uwanja wa Mao Tse Tung linalotarajiwa kujengwa Uwanja Mpya na wa Kisasa ukiwa na viwanja vya ndani vya michezo mbalimbali unaotarajiwa kuaza Mradi huo wa ujenzi katika mwezi huu baada ya kukabidhiwa kwa Kampuni inayojenga uwanja huo kutoka China.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Ndg Omar Hassan King akionesha mchoro wa kisasa wa Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Mao Tse Tung unaotarajiwa kuaza ujenzi wake hivi karibuni baada ya kukamilika kwa taratibu zote za ujenzi huo.na Kuchukua miezi 14 ya ujenzi wake unaojengwa na Kampuni ya Kichana ya Zhengtal Group Company LTD. mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Ndg Omar Hassan King akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya michezo Zanzibar kuhusiana na Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Mao Tse Tung Zanzibar unaojengwa na Serikali ya China kwa Msaada na utagharimu Dola za kimarekali Milioni Tano na nukta mbili sawa na fedha za Kitanzania Milioni 11.5, na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itagharamia zaidi ya shilingi bilioni 1.Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajun Zanzibar.
No comments:
Post a Comment