Habari za Punde

Rais Dk Shein, Ahudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Nchi Zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA) Nchini Indonesia.

Viongozi Wakuu wa Nchi mbali mbali wakiwa katika Picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) uliofanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia,ambapo Rais Dk.Shein (wa tatu kulia)anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli katika mkutano huo

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa kwanza wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli,mkutano huo ulifanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia,(kushoto) Rais wa Sychells Mhe,Danny Faure.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Ussi (katikati) wakiteta jambo wakati wa vikao mbali mbali katika mkutano wa kwanza wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli,mkutano huo ulifanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia,(kushoto) Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe,Hamad Rashid Mohammed na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe,Susan A,Kolimba,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Indonesia Joko Widodo,ambae ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) kabla ya kuanza kwa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia,Rais Dk.Shein anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli
Rais wa Indonesia Joko Widodo,ambae ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) akisalimiana na Rais wa Msumbiji Philipe Nyusi wakati wa mkutano IORA uliofanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia ambao ulihudhuriwa na Viongozi wakuu wa Nchi mbali mbali ,[Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.