Habari za Punde

Waziri wa afya afungua kongamano la kimataifala NED hospitali kuu ya Mnazimmoja

 Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib akiwaeleza washiriki wa Kongamano la Kimataifa la NED Historia na Maendeleo ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja pamoja na kuanzishwa kituo cha NED mwaka 2015.

  Rais wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu inayohusiana na upasuaji wa mishipa ya fahamu, uti wa mgongo na vichwa maji NED) Dkt. Hosea Piquer akitoa maelezo kwa washiriki wa Kongamano la Kimataifa la madaktari wanaoshughulikia maradhi hayo kutoka Afrika, Ulaya na Marekani.

 Mratibu wa Kongamano la Kimataifa la NED linalofanyika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Mahmood Qureshi akizungumza na washiriki wa Kongamano hilo
 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu linalowashirikisha madaktari wa maradhi ya mishipa ya fahamu, uti wa mgongo na vichwa maji NED katika kituo cha maradhi hayo Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Kituo cha NED cha Hospitali Kuu ya Mnazimmoja panapofanyika Kongamano la siku tatu la wataalamu wa maradhi hayo kutoka mataifa tisa ya Afrika, Ulaya na Marekani.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.