Habari za Punde

Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Azindua Bodi ya Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC

Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe Rashid Ali Juma akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya ZBC baada ya kuizundua Bodi hiyo katika Ukumbi wa ZBC Redio Rahaleo na kuitaka kufanya kazi zake kwa ueledi ikizingatiwa imeundwa na Watu mahiri wealiobobea katika Sekta ya Habari ikiongozwea na Mwenyekiti wake Bi Nasra Mohammed Hilal, ambae alikuwa mtangazaji wa siku nyingi katika sekta ya habari Zanzibar.  
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Bi Nasra Mohammed Hilal akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Bodi yao iliozinduliwa na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma katika ukumbi mdogo wa ZBC Redio Rahaleo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Bi. Aiman Duwe akiwa katika ukumbi wa mkutano wa uzinduzi wa Bodi ya Shirika lake. akiwa na Wajumbe wa Bodi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Habari akitowa nasaha zake.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.