Habari za Punde

Kikosi cha Umisseta kanda ya Unguja hadharani, kuenda Mwanza June3



Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kocha msaidizi wa timu ya soka Kanda ya Unguja Abdul wahab Dau “Mwalimu Dau” ametangaza kikosi kipya wachezaji 22 cha timu hiyo ambacho kinatarajiwa kwenda Butimba Jijini Mwanza  katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA)yanayotarajiwa kuanza  June 6, 2017.

Wachezaji hao 22 watachujwa 4 na kubakia 18 ambao watakaokwenda katika Mashindano, mchujo wa mwisho unatarajiwa kufanywa siku chache kabla ya safari.

Kikosi hicho cha wachezaji 22 wa kanda ya Unguja Walinda mlango ni:-

Aley Ali Suleiman (Ubago) na Abass Wadi (Philter)
Wachezaji wengine ni Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki), Amani Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ali Mohd Seif (Tumekuja), Ali Issa (Lumumba), Jamali Ali Jaku (Kinuni), Elias Suleiman (K-pura) na Abdurahman Seif Bausi (Glorious).

Wengine ni Ibrahim Faraj (Lumumba), Faki Kombo (JKU Mtoni), Haji Suleiman (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan (Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Walid Abdi (Mwera), Mansour Mohd (Mtoni), Abubakar Khamis (Bububu), Abdulatif Mzee (Philter), Habibu Ali (Nyerere), Ibrahim Abdallah Hamad (Arahman) na Yakoub Kiparo (Langoni).

Mashindano ya UMISSETA yanayotarajiwa kuanza June 6, 2017 huko Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza ambapo kwa mwaka huu Zanzibar itashiriki kanda mbili tofauti, yani Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.