Habari za Punde

Mlinzi kinda wa Taifa ya Jang'ombe ajumuishwa kwenye kikosi cha Rolling Stone



Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mlinzi wa kati wa Timu ya Taifa ya Jang’ombe Ali Juma Maarifa “Mabata” amejumuishwa kwenye kikosi cha kombain ya Mjini Unguja ambacho kinajiandaa na Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone yanayotarajiwa kufanyika mwezi July mwaka huu jijini Arusha.

Mabata ni miongoni mwa walinzi wadogo wanaocheza ligi kuu soka ya Zanzibar lakini shughuli yake uwanjani tofauti na umri wake ambapo miaka yake chini ya miaka 17 ataungana na wachezaji wengine wa kombain hiyo inayofundishwa na kocha Mohammed Seif “King”.

Nyota wengine waliyoitwa hivi karibuni kwenye kikosi hicho ni Ibrahim Abdallah Ali “Mkoko” wa Miembeni ambae hivi karibuni amerejea Visiwani Zanzibar akitokea mjini Gentil, Gabon katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya AFCON akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania “Serengeti Boys” baada ya kutolewa kwa kufungwa 1-0 na Niger katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, nchini Gabon.

Wengine ni Aley Ali Suleiman “Manula” Mlinda mlango namba moja wa Miembeni city pamoja na Juma Ali Yussuf “James” wa Villa United.

Mbali ya wachezaji hao wapya waliyoitwa kwenye kikosi hicho pia kuna nyota wengine wapya waliyobeba ubingwa msimu ulopita wamerejeshwa kukipa nguvu kikosi hicho.

Wachezaji hao ni Mlinzi wa kushoto wa Black Sailors Muharami Khamis “Terra” pamoja na mlinzi wa kulia wa KVZ Abdul hamid Salum “Ramos” ambapo kwasasa kikosi hicho kitakuwa na wachezaji 25 kwa ujumla.

Wachezaji hao wataungana na wale waliyotangazwa awali wiki mbili zilizopita ambao ni:-

Walinda Mlango Peter Dotto Mashauri (Schalke 04) na Makame Mkadar Koyo (Huru).

Wachezaji wa ndani ni Hassan Chalii (Kipanga), Abdul-halim Ameir (King Boys), Shaaban Pandu (Villa United), Idrissa Makame (Villa FC), Ramadhan Simba (Calypso), Ali Hassan (Uhamiaji), Fahmi Salum (Mlandege), Salum Omar (Villa United), Yakoub Omar (Jang’ombe Boys) na Mohd Ridhaa (Villa United).

Wengine ni Mohd Jailan (Chrisc), Makame Masoud (Schalke 04), Mohd Mussa (Mapembeani), Abrahman Juma (KMKM), Mohd Haji (Jang’ombe Boys), Abdul-hamid Juma (ZAFSA) na Ibrahim Chafu (Villa FC).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.