Habari za Punde

Nasaha za Bi Hekima: Tuwafundishe watoto kuomba radhi wanapokosea. Wazazi wasiwaombee kwa niaba yao!

  Na Bi Hekima
                     
 Ulezi wa watoto wa kiswahili una mashaka  kutokana na ufinyu wa mbinu na ufahamu wa dhana ya ulezi ya walezi wao. Kuna mambo mengi yanayotokea yamenifanya niaminikuwa tatizo kubwa la watoto tunaowaona 'hawana adabu' au 'wameshindikana' ni wazazi na walezi wao. Mzazi au mlezi si lazima awe kamzaa mtoto bali ana mahusiano ya kuwa mkubwa kiumri na kirika kuweza kumuongoza mtoto.

Majuzi niligongwa na kijana. Yeye anadai hajatambua kuwa kanigonga ingawa mwisho wa siku mguu wake ulikua jui wa wangu.na bado hajaona au kuhisi kamkanyaga mtu. Itakavyokua ndo kankanyaga nlitaka kujua ana mpango gani juu ya hilo. Jibu lake ujuba na ubishi. Hajaona kuwa kakosea hata kama hajadhsmiria na kuomba msamaha kwake ilikua dhambi. Nilipokuwa nafanya jitihada za kumfahamisha akatokea babu moja na mvi zake akinizuia kutoa maelekezo kwa kuimba 'basi, imetosha! Basi msamehe! Nenda dada, nenda mama basi mwache!

Hii si.mara ya kwanza kukutana na hali kama hii ambapo najaribu kumtanahabisha kijana juu ya mwendo wa kwenda akatokea 'babu' au mtu anayeingilia na kusambaratisha jitihada hizo ama kwa maksudi au kwa kuamini ndo anaepusha balaa. Madhara ya tabia hii ya kilimbukeni ni kuwa vijana hawapewi haki yao ya kuongozwa, ya kufahamishwa mwenendo gani unafaa au la.

Hali hii pia.iko kwa watoto. Juzi nikirudi nyumbani wakati wa mvua ya jioni maeneo ya Afrika House. Kulikuwa na watoto wamesimama nje na mmoja alikua kashika kama kikopo. Nilipopita karibu yake akafanya kama kunirushia kikopo hicho mbele ya uso wangu. Nkasimama nkiwa nimeshangaa na najaribu kutizama anataka kufanya nini. 

Binti yule aliponiona nimesimama akacheka na kukimbilia ndani kwao. Nikamfuata. 

Nilipofika mlangoni nliona kuwa kuna mwanamke kijana kakaa kibaraza cha ndani anazungumza na simu. Bila ya kukata simu akamuuliza 'umefanya nini?' Akaniliza na mm 'kakufanya nini?' Huku anatabasamu na yupo bado anazungumza na simu. Nkamwambia muulize mwenyewe. 

Wakati narudia kuwa aulizwe mtoto akatoka bibi mmoja kizee ndani...naye akataka kujua kuna nini. Mtoto mwenzake (tena mwenye matatizo ya akili akamfahisha mwenzake lafanya nini. Bibi mtu akaniomba msamaha akitaka yaishe niende zangu. Baada ya kumuamkia mzee huyo, Mimi nkamjibu yeye siye aliyenikosea hivyo hana sababu ya kuniomba msamaha na aliyenikosea yupo mbele yangu ila sijui kama anatambua kuwa alichofanya si sahihi. 


Tena bibi akanimba nimsamehe niende. Wakati huo akatokea mama mwengine kwa ndani naye akitaka kujua kuna nini. Aliwagomba watoto kuwa anawakataza 'kuwarushia watu maji' kila sk. Tena akaomba yeye msamaha na mimi tena nkamfahamisha aliyenikosea ndio wa kutambua kuwa kafanya sivyo na aombe msamaha. 

Hakuna aliyetaka kumuachia mtoto wa miaka 9 ajifunze kutoka 'ujinga' alioufanya. Sauti zao ziliivyoźidi nikawakumbusha toka nimefika sijamtukana mtu au kummpiga mtu. 
Dhumuni langu ilikuwa kumuelewesha mtoto afahamu tabia zinazokubalika na watu usiowafahamu tena wanaoweza kuwa bibi zake ila nimekutana na wazazi ambao kwa mdomo wanaweza kugomba lakini kwa tabia hawaonyeshi umakini wa ulezi.

 Hawezi mtu akaingia kwako kutokana na suala la mtoto usibanduke kwenye simu kumsikiliza tena maongezi ambayo yalikuwa yakishikaji tu! Aidha haiwezekani mtu akawa ana 'issue' na kitendo cha mtoto jibu likawa kumuondoa aliyekuja kwa kuomba radhi kwa niaba ya mtoto. Au kuomba radhi ili 'yaishe'.

Tabia kama hizi haziwafundishi watoto kufahamu wajibu na kuwajibika kwa makosa yao. Pia hawawasaidii.watoto kufahamu nini kinakubalika nini hakikubaliki.

Kesho kijana/mtoto huyu tutataraji aweze ku'cope' kazini, mafunzoni au katika familia yake? Si rahisi. 

Wazee wa zamani wakionya suala la wazazi/walezi kuwahusudu watoto wao. Huu ni mfano mmoja wa wazi. Tusilaumu watoto 'wasipolelewa na kijiji' kama kaya haijinasibu na wanakijiji au na maadili ya kijiji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.