Habari za Punde

Balozi Seif akagua maeneo yalioathirika na mawimbi la Maji ya Bahari katika Pwani ya Mtoni.

 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi  Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud kati kati akimuonyesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi maeneo yalioathirika na mawimbi la Maji ya Bahari katika Pwani ya Mtoni.
 Balozi Seif Ali Iddi akikagua baadhi ya maeneo yaliyoathirika na kasi ya maji ya Bahari na kusababisha mmong’onyoko wa ardhi ulioathiri baadhi ya Nyumba za Mtaa huo wa Asili.
 Sheha wa Shehia ya Mtoni Bwana Hassan Zaid Ali wa kwanza kutoka Kushoto akielezea athari za mmong’onyoko wa ardhi zinazolikumba eneo la Pwani ya Mtoni toke asili.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tathmini ya Athari za Kimazingira Ndugu Ali Vuai Pandu akitoa ufafanuzi wa tathmini ya awali iliyofanywa na Wataalamu wa Kitengo chek katika eneo la Pwani ya Mtoni mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Mzee wa Mtaa wa Pwani ya Mtoni Bwana Yussuf Amour Abdulla akimueleza Balozi Seif  changamoto zinazowakumba Wananchi wa eneo hilo za kuongezeka kwa kina cha Maji ya Bahari na kuathiri makaazi yao.


Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.