Habari za Punde

Hali Ilivyokuwa Katika Marikiti Kuu ya Darajani Maandalizi ya Sikukuu ya Eid el fitr Zanzibar.

Wananchi wa Zanzibar wakiwa katika harakati jana kukamilisha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kutafuta mahitaji ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitry baada ya kukamilika kwa Ibada la mfungo na kujimuika na Waislamu Wengi Duniani kuadhimishi Siku hiyo.
Wananchi wakiwa katika marikiti kuu ya darajani wakinunua viazi mbata kilo moja iliuzwa kwa shilingi 900/= na 1000/= kwa kilo moja katika marikiti hiyo tungule kilo moja imeuzwa shilini 2000/= na vitunguu maji kilo moja vimeuzwa shilingi 2000/= kwa kilo. 
Hali ilivyokuwa marikiti kuu ya darajani jana kuhitisha mfungu wa ramadhani.  

Wafanyabiasha ya kuku katika marikiti kuu ya kuku darajani jana kuku mmoja wa kishwahili ameizwa kati ya shilingi 20,000/= na 25,000/= kutegemea ukubwa wa kuku na kuku wa kizungu wa mayai ameuzwa shilingi 12,000/ na wa nyama ameuzwa shilingi 7000/ na 6500/=.
Wafanyabiasha ya kuku katika marikiti Kukuu ya darajani wakiwa na kuku hao wakiuza kwa shilingi 20,000/=

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.