Habari za Punde

Jangombe Boys Kuwapa Mazoezi Kombaini ya Mjini Kesho.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Jang'ombe Boys kesho  Jumatano saa 3 za usiku katika uwanja wa Amaan.

Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja kwa majukwaa ya kawaida na V.I.P ni shilingi Elfu mbili.

Kombain ya Mjini wanajiandaa na Mashindano ya Rolling Stone yanayotarajiwa kuanza July 9 hadi July 19, 2017 huko Mburu Manyara wakati Jang'ombe boys wanajiandaa na kuendelea kucheza hatua ya 8 bora ligi kuu soka ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.