Habari za Punde

Wazanzibar Wengine 2 Kutaka Kusajiliwa Kigi Kuu ya Bara.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.   
               
Kocha mkuu wa timu ya Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali Bushir “Bush” amepania kufanya usajili wa wachezaji wane wapya kwa nafasi tofauti wakiwemo Wazanzibar wawili.

Bushir amesema amepania kusajili wachezaji wa nne akiwemo Mlinda Mlango na Kiungo mkabaji kutoka Ligi kuu soka ya Zanzibar na wengine wawili ni Kiungo mshambuliaji na Mshambuliaji wa kati kutoka Ligi kuu soka ya Tanzania Bara.

Amesema tayari ameshaanza mazungumzo na Wachezaji hao lakini kwasasa bado hajaweka wazi majina yao.

“Nimepania kusajili wachezaji 4 tu katika dirisha hili, nafanya hivyo kwa vile wachezaji wangu wengi wameshanifahamu vyema taaluma yangu ndio maana nitasajili wane tu ili kuja kuongezea nguvu tu, wachezaji ambao nimeshaongea nao ni mlinda mlango na kiungo mkabaji kutoka ligi kuu ya Zanzibar, na wengine ni kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wa kati mmoja hawa wote kutoka ligi kuu ya bara, majina kwasasa sitowataja kwa vile nishapeleka ripoti kwa uongozi na binafsi nimeshaongea nao.

 Zanzibar kuna vipaji vingi sana nawaomba vijana wazidi kujituma ili wapate nafasi ya kucheza nje ya Zanzibar na hata timu ya Taifa tutakuwa nayo nzuri ukiangalia na sasa sisi Zanzibar ni wanachama wa CAF”. Alisema Bushir.

Kocha Bushir alitokea KMKM ya Zanzibar na  alijiunga na Mwadui FC msimu ulopita katika dirisha dogo na kufanikiwa kumaliza nafasi ya 10 katika ligi hiyo ambapo aliichukua timu hiyo ikiwa ipo nafasi ya 15 nafasi ambayo ni ya pili kutoka mkiani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.