Habari za Punde

Makamu wa Rais Mama Samia Azindua Zoezi la Ugawaji wa vifaa kusaidia akina mama wajawazito

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla maalum ya kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati na baada ya kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo mabeseni 100 yenye vifaa hivyo kati ya 1000 yalikabidhiwa kwa hospitali ya Mbagala Rangi Tatu, Dar Es Salaam.
 Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem akihutubia mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100,Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Baadhi ya mabeseni yenye vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania wakiangalia mbabeseni yanya vifaa vya kusaidia wakina mama kujifungua yaliotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bi.Arafa Nurdin wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala Rangi Dkt. Joseph Kiani wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsalimia mtoto mwenye miezi miwili Jenifer Mathias, kulia ni baba wa mtoto Bw. Mathias Miano mkazi wa Kingugi, Mbagala kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
 Sehemu ya wananchi wa Mbagala Kizuiani kwenye kituo cha Afya cha Mbagala Round Table waliojitokeza kumsikiliza  Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar.
                           .............................................................. 
     Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua zoezi la ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba 200 yaliyotolewa na Ubalozi wa Kuwait nchini kwa ajili ya wanawake wajawazito katika hospitali ya Mbagala Rangi Tatu  na Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Lengo la mpango huo ni kutoa mabeseni hayo zaidi ya 1,000 kwa wanawake wajawazito wasio na uwezo kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar kama hatua ya kukabiliana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito nchini.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vifaa tiba hivyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mpango huo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupambana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito kwa kukosa vifaa tiba kutokana na umaskini unaowakabili.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kwa maeneo yaliyopatiwa mabeseni yenye vifaa tiba yahakikishe vifaa hivyo vinatolewa kwa wanawake wajawazito ambao baadhi yao wanakata tamaa kwenda kujifungulia kwenye hospitali au kwenye vituo vya afya  kwa kukosa vifaa hivyo kwa sababu ya umaskini.

Amesema mkakati uliopo wa Serikali ni kuhakikisha huduma za afya nchini zinaendelea kuboreshwa hasa huduma ya mama na mtoto ambapo kutokana na umuhimu wa sekta ya afya Serikali imetenga fedha za kutoka katika bajeti ya mwaka 2017/2018.


Makamu wa Rais ameeleza kuwa mradi huo wa ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba katika mradi huo kuanzia sasa utasimamia na wake wa viongozi wastaafu na wakiwemo wake wa mawaziri baada ya kuuzindua rasmi.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa msaada wake huo ambao amesema utakuwa ni chachu ya kupambana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa upande wake, Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amesema Serikali ya Kuwait kupitia kwa Jumuiya ya Red Crescent ya nchini hiyo itaendelea kusaidia vifaa tiba mbalimbali kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu na maeneo yao.

Balozi huyo wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amesisitiza kuwa milango ya ubalozi wa Kuwait ipo wazi kwa Taasisi mbalimbali za Kiserikali kupeleka maandiko mbalimbali kwa ajili ya kuomba kupatiwa misaada lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma za viwango vya juu katika sekta mbalimbali.

Amesema kwa sasa Serikali ya Kuwait ipo mbioni kutiliana saini ya makubaliano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo Unguja.

Ameeleza kuwa ukarabati huo utaiwezesha hospitali hiyo kuongeza utoaji wa huduma bora kwa wananchi wengi zaidi.

Halfa ya makabidhiano ya mabeseni 200 ya vifaa tiba katika hospitali ya Mbagala Rangi Tatu na Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam imehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.