Habari za Punde

Kocha Burhan Msoma Aibuka Tena Katika Medali ya Soko Zanzibar. Na Kupania Kuleta Mabadiliko katika Soko Zanzibar.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kocha wa zamani wa Simba, Kagera Sugar,Nairobi, Kenya Army, Fesal Sports Club, Forodha, Kikwajuni na Bandari, Burhan Msoma amerejea kwenye soka na sasa ni kocha mkuu wa klabu ya Gulioni FC inayoshiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini.

Msoma ambae amefundisha soka kwa mafanikio hasa katika klabu ya Simba mwaka ya 2004 na kufanikiwa kufika hatua ya Robo fainali ya kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, ametoboa siri ya kurejea tena katika soka ambapo amesema siri kubwa baada ya kuona soka la Zanzibar limedorora ndipo alipoamua kurejea baada ya kushawishiwa na Gulioni.

Amesema ameona soka la Zanzibar linazidi kupotea ndipo aliposhawishiwa na Abdul Mshangama kurejea tena nae akakubali ili akalikombowe ambapo amepania kulikomboa soka hilo.

“Ni kweli nimekaa miaka mingi sana soka la Zanzibar silitaki hata kulisikia, lakini sababu kubwa ilonifanya nirejee kufundisha baada ya kushawishiwa na Abdul Mshangama kwenda kufundisha Gulioni, nikaamua bora nije kulikomboa soka la Zanzibar mana mbali ya Mshangama kuna wengi wamenishawishi nirudi katika soka akiwemo ndugu yangu Abdulghan Msoma, Chile na wengine wamenambia njoo hamasishe soka sasa linarudi katika ubora wake, namimi nikaamua kurudi”.
Timu yake Msoma Gulioni leo saa 10 za jioni itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini mchezo ambao utasukumwa katika uwanja wa Amaan.

Mbali na mchezo wa leo pia Gulioni watacheza mchezo mwengine wa kirafiki sikukuu ya Eid ya Pili dhidi ya Taifa ya Jang’ombe saa 2:00 za usiku katika  uwanja wa Amaan, kisha kucheza tena sikukuu ya Nne dhidi ya Jang’ombe Boys saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.