Habari za Punde

Ninja wa Yanga awaaga Wazanzibari, atoa maneno mazito Uwanja wa AmaanNa: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mlinzi mpya wa Yanga Abdallah Haji Shaibu "Ninja" amewaaga mashabiki wa soka Visiwani Zanzibar na kuwaomba wamsamehe kama aliwakosea kwa kipindi chote alichocheza soka Visiwani hapa.

Akiwaaga Mashabiki hao jana usiku katika uwanja wa Amaan kwenye mchezo maalum wa uzinduzi wa COCO SPORTS NDONDO CUP ambapo Taifa ya Jang’ombe walipigwa 2-1 na Mlandege, Ninja amewashukuru Makocha wake wote tangu alipokuwa mdogo mpaka kufika Taifa ya Jang’ombe.

Aidha Ninja amewaomba Mashabiki hao wamsamehe kama aliwakosea kwa kipindi chote huku akiwataka wazidi kumuombe dua ili afanikiwe katika Maisha yake mapya ya Jangwani.

“Kwanza Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kusajiliwa Yanga, la pili na nawashukuru Makocha wangu wote tangu walonifundisha kuanzia Juvenile, Junior na Central, la tatu nawashukuru Mashabiki wangu wa Taifa ya Jang’ombe kwa kunisapoti, na pia nawaomba Wazanzibar kama kuna mtu nimemkosea anisamehe na mimi nimeshawasamehe wote, hivyo muniombe pia dua kwa Mungu anisaidie kwani lengo langu si kucheza Yanga bali kucheza nje ya Tanzania”. Alisema Ninja.

Ninja ndie mchezaji wa kwanza msimu huu wa mwaka 2017-2018 kusajiliwa Yanga akitokea Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar ambapo amefunga mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.