STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 13.06.2017
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Viongozi wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar (SMZ), aliowateua hivi karibuni kuwa Wakuu katika Vikosi hivyo.
Katika hafla hiyo, Dk.
Shein kabla ya kumuapisha Naibu Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Ali Abdalla Ali,
alimfisha cheo cha Ukamishna na baadae kumuapisha kuwa Kamishna wa Chuo cha
Mafunzo, Zanzibar.
Wakati huo huo, Dk.
Shein, amemuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la
Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU).
Hafla hiyo, ilifanyika
Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa
Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali
Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar
Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said,
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za (SMZ), Haji Omar
Kheir, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid
Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa
Zanzibar Sheikh Khamis Haji.
Wengine ni Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed
Mahmoud, Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Meya
wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa
Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment