Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein Atunuku Nishani leo.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                                                                                                29.06.2017
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  amewatunuku nishani viongozi na Wananchi mbalimbali ambao waliitumikia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Nyanja mbalimbali. 

Ghafla hiyo ya utunuku wa nishani hizo ilifanyika ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Wananchi. 

Dk Shein alitoa nishani hizo kwa viongozi na wananchi 52 ikiwemo nishani ya Mapinduzi  12, ambayo hutunukiwa viongozi wenye sifa za kipekee, nishani ya utumishi uliotukuka 20 na nishani ya ushujaa 20. 

Waliotunukiwa nishani ya Mapinduzi ambayo hutolewa kwa mtu ambaye alisisi au alishiriki au aliyatukuza na aliyeyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, ambapo nishani hii hutunukiwa kwa makundi mawili likiwemo kundi la viongozi wenye sifa za kiepee ambao ni aliyekuwa Makamu wa rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Omar Ali Juma na Marehemu Ali Muhsin Ali aliekuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi. 

Wengine waliotunukiwa nishani ya Mapinduzi  viongozi na wananchi wenye sifa maalum ni Pandu Ameri Kificho Spika mstaafu wa Baraza la Wawakilishi , Aboud Talib Aboud Mjumbe mstaafu wa baraza la Mapinduzi,Dk  Msimu Abdulrahman Hassan,Mastura Ali Salim na Zainab Omar Mohamed. 

Wengine waliotunukiwa nishani hiyo ni Thereza Olban Ali,Marehemu Makame Mzee Suleiman,Marehemu Isaac Abraham Sepetu,Marehemu Asha Bakari Makame na Marehem Hamid Vuai Mkungu. 

Aidha, Dk Shei aliwatunuku nishani watumishi wa Serikali, Mahkama na Baraza la Wawakilishi ambao aliwatunuku nishani ya utumishi uliotukuka. 

Watunukiwa hao ni Jaji Hamid Mahmoud Hamid, Mohammed Fakih Mohamed, Mohamed Ahmed Mohamed, Ali Rajab Juma, Mwanaidi Saleh Abdallah, Maoud Mohamed Ali Shambi, Mwapili Mohmoud Mzee, Josefrida Gloria Parwira na Marehemu Mohamed Jongo. 

Akitoa tamko la kwanza  katika shughuli hiyo ya kutunuku nishani katika ghafla hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Salum Maulid Salum, alisema kuwa waliotunukiwa nishani hizo  sifa zao zimekidhi matakwa ya nishani.
Alisema kuwa kwa kutumia uwezo wake Rais Dk. Shein al;iopewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Mambo ya Rais namba 5 ya mwaka 1993, na ilivyotangazwa katika Tangazo la Kisheria namba 67 kupitia Gazeti Rasmi la Serikali. 
 
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.