Habari za Punde

Sakho wa Timu ya Liverpool Atembelea Kituo cha Watoto Yatima cha SOS Zanzibar.

Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar wakiwa na mabango ya kumkaribisha Mchezaji wa Timu ya Liverpool Mamadou Sakho katika viwanja vya Kijiji chao mombasa Zanzibar kuwatembelea na kukabidhi msaada wa Vyakula kwa Watoto hao akiwa na Mke na Watoto wake.
Mchezaji wa Timu ya Liverpool Mamadou Sakho akisalimiana na Watoto wa Kijiji cha Watoto SOS mombasa Zanzibar alipowasili katika kijiji hicho kuwatembelea watoto hao na kukabidhi vyakula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitry wiki ijayo kuweza kujumuika na watoto wenzao kufurahiyi sikukuu hiyo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mchezaji wa Timu ya Liverpool Mamadou Sakho akiwa katika picha ya pamoja na Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa Watoto hao wanaoishi katika Kijiji hicho. 








Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Familia ya beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England jana jioni  ametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS kilichopo Mombasa Unguja.

Sakho amefatana na mke wake Madna na Watoto wake wawili wa kike.
Jana Ijumaa saa 3:00 za usiku katika uwanja wa Amaan Sakho amezindua Mashindano ya COCO SPORTS NDONDO CUP katika uwanja wa Amaan, mchezo ambao Taifa ya Jang’ombe walifungwa 2-1 na Mlandege SC.

Sakho yupo hapa Viswani Zanzibar tangu Jumamosi June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja Jumamosi kufika hapa Zenj.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.