Habari za Punde

Balozi Seif atembelea Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dara es salaam

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dara es salaam Bara bara ya Kilwa Jijiji Dar es salaam. Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Slum Ali na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Nd. Felix Lyaniva.
Balozi Seif akikagua Bidhaa katika Banda la Shirika la Miga Chaa Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lilioo kwenye maonyesho ya 41 ya Biashara Dar es slaam
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiangalia bidhaa za vifaa vya kupikia jikoni kwenye banda la Wafanyabiara kutoka Nchini Misri. 
Balozi Seif akitoka nje ya baada ya kuangalia Banda la Bidhaa za Wafanyabiashara, Taasisi na Wajasiri amali wa Zanzibar
Balozi Seif Kulia na Waziri wa Biashara na Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali wakiangalia bidhaa mbali mbali za kanga na vitenge vilivyotengenezwa na Tanzania Textile Limited.
Balozi Seif akiwalishia Samaki wanaofugwa kwenye Bwawa la Banda la Jeshi la Kujenga Taifa Tanzania {JKT} kwenye Mabanda ya Maonyesho ya Kimataifa ya Dar es salaam. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na washirika wa Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa Dar es salaam baada ya kutembelea mabanda mbali mbali

Na Othman Khamis, OMPR

Makamu wa ili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaagiza Wazalishaji wa bidhaa za Viungo kujitahidi kuongeza nguvu za uzalishaji wa Kilimo cha Viungo ili kuirejeshea hadhi yake Tanzania ya kuongoza katika uzalishaji wa Bidhaa hizo Duniani. 

Alisema wazalishaji hao ni vyema wakazingatia pia ushauri na maelekezo ya Wataalamu pamoja na Viongozi katika kuona Kilimo cha mazao ya Viungo kinaimarika na kuleta tija. 

Balozi Seif AlI Iddi alitoa agizo hilo mara baada ya kuyatembelea mabanda mbali mbali ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Uendelezaji Biashara Tanzania {Tan Trade} kwenye Viwanja vya Julius Nyerere Bara bara ya Kilwa Jijini Dar es salaam. 

Tarehe 10 Julai 2107 ni siku maalum ya Bidha mbali mbali za Viungo kwenye Maonyesho hayo {Spice Day } yanayotembelewa na zaidi ya Wananchi na Wageni wapatao Laki Moja kwa Siku. 

Balozi Seif alisema yapo masoko mengi Duniani hasa Nchi zilizoko katika ukanda wa Bara ya Asia yanayohitaji kufanya Biashara za bidhaa zinazotokana na Viungo jambo ambalo wazalishaji hao wanaweza kuitumia fursa hiyo katika kuongeza kipato. 

Alisema kwa vile bidhaa za Viungo zitaendelea kuwa muhimu katika Maisha ya Bianaadamu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zitashirikiana katika kuona maonyesho ya bidhaa tofauti yanayokuwa yakifanyika kwa pande zote mbili yanafanikiwa. 

Makamu wa Pili wa Frais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Mamlaka ya Uendelezaji Biashara Tanzania { Tan Trade } pamoja na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Tanzania Bara kwa uamuzi wao wa kutenga siku maalum kwa bidhaa maalum ndani ya Maonyesho hayo ya 41 ya Biashara Dar es salaam. 

Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam ya Mwaka huu yamefana sana kutokana na utaratibu mzuri wa bidhaa kutengewa siku Maalum ”. Alisema Balozi Seif. 

Mapema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam { Tan Trade } Nd. Edwin Rutageruka alisema Nchi 30 Duniani zilizojumuisha Makampuni 515 na yale ya Wazalendo yapatayo 2,520 yameshiriki kwenye Maonyesho hayo ya Kimataifa Dar es salaam. Nd. Rutageruka alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Mikataba ipatayo Milioni 2,000,000 inatarajiwa kusainiwa mara baada ya kumalizika kwa maonyesho hayo ya Kimataifa . 

Alisema zaidi ya wananchi na Wageni mbali mbali wapatao Laki 100,000 hutembelea mabanda mbali mbali kwa siku kujionea na kujipatia huduma kulingana na mahitaji yao. Akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuzungumza na wadau mbali mbali wa Maonyesho hayo 

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali alisema Tanzania ilikuwa na sifa kubwa ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na Viungo Duniani.
Alisema sifa hiyo inapaswa kuchukuliwa juhudi za ziada kwa pande zote mbili za Tanzania Bara na Zanzibar ili iweze kuongoza tena hasa kipindi hichi kinachoelekea katika Tanzania ya Viwanda. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika ziara hiyo ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam alitembelea mabanda ya Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri, Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Banda la Shimono la Singapore pamoja na lile la shirika la Taifa la Biashara Zanzibar {ZSTC}. 

Mengine ni Z.H. Group, Mahanjumati, Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Zaindan Chukwani Zanzibar, Jiko la Shamba Ndijani, Banda la Viwanda Vidogo vidogo {SIDO}, Bakharesa Group,Metl, Mfuko wa Fursa sawa kwa wote, Jeshi la Kujenga Taifa {JKT}, Wizaya ya Viwanda Biashara na Uwekezaji pamoja na Banda la Bidhaa za Viungo. Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 9/7/2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.