Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama
Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, akiongoza maandamano ya Mabalozi wa Usalama Barabarani
kuingia Uwanja wa Mashujaa, wakiadhimisha siku yao iliyofanyika kitaifa mkoani
Dodoma leo.Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed
Mpinga
Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama
Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa
Usalama Barabarani ambapo aliwaasa madereva kufuata sheria ili kuweza kupunguza
tatizo la ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kuacha idadi
kubwa ya wahanga wa ajali hizo.Wapili
kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP
Mohamed Mpinga na anayefuatia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma,Lazaro
Mambosasa. Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani
Dodoma
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani ambae pia ni Mkuu wa Kikosi
cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga, akizungumza wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwaasa askari wa
usalama barabarani kusimamia sheria ili
kuweza kupunguza tatizo la ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha
vifo na kuacha idadi kubwa ya wahanga wa ajali
hizo.Kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye
pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na
kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa. Maadhimisho hayo
yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma,Lazaro
Mambosasa akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama
Barabarani ambapo aliwashukuru mabalozi hao kuchagua mkoa wa Dodoma kufanyia
maadhimisho hayo na kuahidi kuelimisha watumiaji wa vyombo vya moto sheria na
kanuni za usalama barabarani ikiwa anaongoza mkoa ambao ni Makao Makuu ya nchi .Wakwanza
kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza
la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani ambae pia ni Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga.Maadhimisho hayo
yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma
Mabalozi wa Usalama wa Barabarani wakifuatilia
hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo
pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo
aliwaasa madereva kufuata sheria ili kuweza kupunguza tatizo la ajali za
barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kuacha idadi kubwa ya wahanga
wa ajali hizo. Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo
mkoani Dodoma
Msanii Faustine Matina ambae ni Balozi wa
Usalama Barabarani, akiimba wimbo wa kuhimiza masuala ya kuzingatia sheria za
usalama barabarani wakati wa Siku ya Maadhimisho ya Mabalozi wa Usalama
Barabarani, iliyofanyika kitaifa leo katika Uwanja wa Mashujaa,mkoani Dodoma
Mhanga wa ajali anayefahamika kwa jina la Mpemba
Asilia, akizungumza na Mabalozi wa Usalama Barabarani, alipofika
katikaMaadhimisho ya Mabalozi wa Usalama Barabarani yaliyofanyika kitaifa leo
katika Uwanja wa Mashujaa,mkoani Dodoma
Mwenyekiti wa Taifa wa
Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watano kulia),akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Mabalozi wa Usalama Barabarani wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama
Barabarani yaliyofanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.Wasita
kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini,DCP Mohamed Mpinga
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment