Habari za Punde

Duru ya Kwanza Ligi Kuu ya Zanzibar Inaaza Kesho na Kumalizika Jumamosi Timu ya JKU Ikiwa Ndio Kinara.

Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.
Mzunguko wa saba wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora utaanza kupigwa kesho Ijumaa 21/7/2017 kwa kupigwa michezo mitatu ambapo mchezo nambari 25 Mwenge vs Taifa Jang’ombe saa 10 jioni Gombani, Mchezo nambari 26 Jang’ombe boys vs Kizimbani saa 10 jioni Amaan na Mchezo nambari 27 JKU vs Jamhuri saa 1:00 usiku Amaan.

Ligi hiyo itamaliza duru ya kwanza Jumamosi 22/7/2017 kwa Mchezo mmoja nambari 28 Okapi vs Zimamoto saa 10 jioni Gombani.

Mpaka sasa timu zote 8 zimeshacheza michezo 6 ambapo katika msimamo JKU ndio kinara akiwa na alama 15 baada ya kushinda michezo 5 na kupoteza mchezo 1 ambapo Jamhuri ikikamata nafasi ya 2 baada ya kushinda michezo 4, sare 1 na kupoteza mchezo 1 wakiwa na point 13 ambapo Jang’ombe Boys wanakamata nafasi ya 3 wakiwa na alama 13 baada ya kushinda michezo 4, sare 1 na kupoteza mchezo 1 huku Zimamoto inakamata nafasi ya 4 kwa alama zao 11 kufuatia kushinda michezo 3, sare 2 na kupoteza 1.

Nafasi ya 5 inakamatwa na Kizimbani ambayo imeshinda michezo 2 na kupoteza michezo 4 wakiwa na alama 6 ambapo Okapi akikamata nafasi ya 6 kwa point 5 baada ya kushinda mchezo 1, sare 2 na 3 kupoteza, wakati huo huo Taifa ya Jang’ombe inashika nafasi ya 7 kwa alama zake 3 kufuatia kwenda sare 3 na kupoteza 3 huku Mwenge akikamilisha nafasi ya 8 baada ya kwenda sare mchezo 1 na kupoteza michezo 5 akiwa na alama yake 1 pekee.

Ikumbukwe kuwa hatua hiyo ya 8 bora ni kwaajili ya kuwatafuta Wawakilishi wa Zanzibar watakaoshiriki Mashindano ya Kimataifa ambapo Bingwa atawakilisha kwenye Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika na mshindi wa pili atawakilisha kwenye Kombe la Shirikisho Barani humo ambapo msimu uliopita Zimamoto na KVZ waliwakilisha Zanzibar katika Mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.