Habari za Punde

Fensi ya Tamasha la 22 la Mzanzibar Visiwani Zanzibar Lawa Kivutio Kwa Wananchi Zanzibar.

Vijana wa Kikosi cha Reki wakisafisha njia wakati wa kupita Fensi ya Tamasha la Mzanzibar la 22, linalofanyika Visiwani Zanzibar kwa kuonesha bidhaa za asili katika viwanja vya Mnara wa Mapinduzi Michezani Zanzibar.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt. Muslim Hijja akipokea maandamano ya Fensi ya Mzanzibar katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michenzani Zanzibar
Vijana wa Kikosi cha Reki wakipita mbele ya mgeni rasmin wakati wa maandamano ya Fensi za Tamasha la Mzanzibar linalofanyika visiwani Unguja na kumalizikia Kisiwani Pembe Wiki ijayo. 
Ndege ya baskeli ikipita katika mitaa mbalimbali wakati wa fensi la Tamasha la Mzanzibar.


Watoto wakiwa katika shughuli za jando wakati wa enzi hizo.
Mila za Wazanzibar wakati watoto wanapotoka jando baada ya kutahiriwa enzi hizo kwa kufuata mila za asili.
Washiriki wa Fensi wakionesha jinsi ya kupunga kwa ngoma ya viwale.

Makaazi ya asili katika vijiji visiwani Zanzibar. 
Enzi za zamani jinsi shughuli mbalimbali visiwani Zanzibar zikifanyika kama kubeba maji kwa mzegazega na kutembea bidhaa kwa mali kwa mali na uuzaji wa kahawa kwa tutembea mitaani na buli.
Msanii Maarufu Zanzibar Halikuniki akionesha jinsi ya upigaji wa chuku kwa njia za asili kwa kutumia pembe za ngombe.














No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.