Habari za Punde

Kombain wilaya ya mjini kucheza na Dulla Boys kesho

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Dulla Boys kesho Jumatatu July 3, 2017 saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.

Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja na V.I.P ni shilingi Elfu mbili.

Mchezo wa mwisho wa kirafiki Mjini watacheza na Kwerekwe City siku ya Jumatano July 5, 2017 saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.

Kombaini ya Mjini wanajiandaa na Mashindano ya Rolling Stone yanayotarajiwa kuanza July 9 hadi July 19, 2017 huko Mbulu Manyara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.