Habari za Punde

Hatimai Mhe. Ulembo Akubali Shinikizo Achukua Fomu Kimyakimya leo Mjini Dodoma.
















Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo akikabidhiwa fomu ya na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dodoma, Gama Juma, leo.

NA MWANDISHI WETU, DODOMA
Hatimaye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo ametii shinikizo lililokuwa likitolewa na Wazee, viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo kumuomba agombea tena nafasi yake.


Hayo yametimia kufuatia Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Alhaji Bulembo kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi hiyo, katika Ofisi za Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dodoma leo mchana, huku akifanya tukio hilo kimyakimya tofauti na ilivyozoeleka ambapo baadhi ya wawania uongozi husindikizwa na wapambe na waandishi wa habari.



Licha ya kwenda kimyakimya, lakini taarifa zilizopatikana mjini hapa, zimesema kwamba alifika kwenye Ofisi za hizo za Wazazi mkoa wa Dodoma mda wa saa nane mchana akijiedesha kwa gari namba T888 DFB aina Toyota Land Cruser lenye vioo vya giza, na kukabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa Jumuia wa mkoa Gama Juma.



Mapema mwaka huu Alhaj Bulembo alitamka katika katika moja ya vikao rasmi vya Jumuiya ya Wazazi kwamba hatagombea tena nafasi yake ya Uenyekiti, kauli ambayo ilidumu kwa mda mrefu lakini baadaye Baadhi ya Wazee akiwemo Balozi Job Lusinde na baadhi ya viongozi na Wanachama wa Jumuia hiyo wakanza kutoa kauli za kumsihi abatilishe uamuzi wake huo wa kutogombea tena.



Maombi hayo yaliripotiwa kutolewa kwa nyakati na sehemu tofauti hapa nchini, wakiwemo Makatibu wa Jumuia hiyo kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar, ambao kwenye Semina moja iliyofanyika mjini hapa, mwezi uliopita, walimsihi Alhaj Bulembo kuchukua fomu huku wakisisitiza kwamba ikibidhi watamlipia fedha za fumu hizo.



Kufuatia mwaka huu wa 2017 kuwa mwaka wa Uchaguzi wa Viongozi ndani Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake ikiwemo Jumuiya hiyo ya Wazazu Tanzania na Jumuia za Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT), UVCCM  kuanzia ngazi ya Tawi hadi Taifa CCM ilitangaza kuanza kutolewa fomu kwa wanaohitaji rudhaa za uongozi kwa ngazi hizo, kuanzia leo Julai 20217.



Kulingana na msimamo wa sasa wa CCM baada ya mabadiliko makubwa iliyofanya Dodoma, ambayo pamoja na kutaka kuwa na viongozi wenye nia za dhati na wenye kuguswa na shida za wananchi, bila shaka wanaowania uongozi katika kinyang'anyiro  cha uchaguzi huo watalazimika kuwa wamejipima vya kutosha kulingana na sifa zilizotajwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.