Waziri wa Mambo ya nje na Ushirkiano wa Afrika
Mashariki Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Mawaziri wa
Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (hawapo pichani) wakati
akifungua mkutano wa 19 wa Kamati hiyo unaojadili ushirikiano katika masuala ya
Siasa, Ulinzi na Usalama mapema hii leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dr. Stergomena Tax
akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano wa 19 wa Kamati ya Mawaziri wa Nchi
zaJjumuiya hiyo inayojadili ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na
Usalama mapema hii leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC) wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya nje na
Ushirkiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (hayupo pichani) wakati
akifungua mkutano wa 19 wa Kamati hiyo unaojadili ushirikiano katika masuala ya
Siasa, Ulinzi na Usalama mapema hii leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha
na Eliphace Marwa – MAELEZO)
Na.
Bushiri Matenda- MAELEZO
Serikali ya Tanzania
imesema itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika (SADC) kuhakikisha kunakuwa na amani na mshikamano miongoni mwa nchi
wanachama wa Jumuiya hiyo.
Akizungumza wakati
akifungua mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Jumuiya hiyo leo Jijijini Dar es Salaam,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.
Augustine Mahiga alisema kuwa Tanzania itaendeleza jitihada zinazofanywa na
SADC kwa nchi wanachama katika kuendelea kuimarisha Ushirikianao katika Siasa, Ulinzi na Usalama.
“Nawasilisha salamu za
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni
Mwenyekiti wetu wa SADC ambaye anaamini kuwa mkutano huu unatuleta pamoja
katika kujenga ushirikiano wetu zaidi kuhakikisha kuwa tunaendelea kuwa na
amani, umoja, mshikamano na ustawi kati ya nchi wanachama,” alisisitiza Dkt.
Mahiga
Dkt. Mahiga alisema
kuwa nchi wanachama zimeendelea kuwa eneo lenye usalama na ustawi kwa
kuzingatia hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na umoja huo kupitia kamati
mbalimbali zilizoundwa kushughulikia mageuzi katika nchi za Lesotho hali
iliyosaidia Taifa hilo kufanya uchaguzi wa wabunge mwezi June 2017 kwa amani.
Aliongeza kuwa katika
mkutano huo watajadili swala la uhuru wa wananchi wan chi wanachama kutokuwa na
vikwazo wanapotaka kuingia nchi nyingine,kuwa na Kikosi maalum cha Jeshi kwa
ajili ya ulinzi wa amani,mikakati ya kusimamia masuala ya mawasiliano na
habari, hali itakoyochochea maendeleo kati ya nchi wanachama.
Pia SADC kwa kuzingatia
kifungu cha 7 (1) cha itifaki ya umoja huo kuhusu mapambano dhidi ya rushwa,
nchi wanachama zitakuwa na sera na mikakati inayofanana katika kupambana na
rushwa kwa kuzingatia mapendekezo ya Kamati ndogo ya mapambano dhidi ya rushwa
yatakayojadiliwa katika mkutano huu.
Katika kutekeleza azma
yakuondoa tatizo la rushwa kwa nchi wanachama Balozi Dkt. Maiga alizitaka nchi
wanachama kuendelea kutekeleza itifaki hiyo katika kutokomeza rushwa katika
nchi wanachama.
Aidha Balozi Maiga
amewaalika wajumbe wa mkutano huo kutembelea vituo vilivyopo hapa nchini
ikiwemo mlima Kilimanjaro, Serengeti, Visiwa vya Zanzibar na Mafia ili kujionea
vivutio vilivyopo katika maeneo hayo.
Kwa upande wake Katibu
Mtendaji wa SADC Mhe. Stergomena Tax amesema kuwa Umoja huo utaendelea
kushughulikia mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, pia amewaomba nchi
wanachama na washirika wa maendeleo kuendelea kuchangia katika Jumuiya
hiyo ikiwemo Umoja wa Ulaya (EU) .
Mkutano wa 19 wa
Mawaziri wa nchi wanachama unafanyika Jijini Dar es Salaam ukilenga kujadili
maswala ya Siasa, Ulinzi, Usalama na Ushirikiano ndani ya Jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment