Habari za Punde

Shirika la Posta Tanzania Laibuka Kidedea Kwa Watoa Huduma Bora Kutoka Taasisi za Umma na Binafsi Kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam

SHIRIKA la Posta na Simu chini ya uongozi mpya, imejinyakulia tuzo ya mshindi wa kwanza wa watoa huduma bora kutoka taasisi za umma na binafsi, zinazoshiriki maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, yaliyofunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Julai 1, 2017. Maonesho hayo ya kila mwaka yameandaliwa na Mamlaka ya Uendelezaji Bishara Tanzania, (TAN Trade). Pichani juu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Deo Kwiyukwa, (katikati), akiwa amekamata tuzo hiyo pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo kwenye banda lao.

Bw. Kwiyukwa (kushoto), akiwakabidhi tuzo hiyo wafanyakazi wenzake baada ya kupokea toka kwa Rais Magufuli.

 Wafanyaakzi wa Shirika la Posta Tanzania, wakiwahudumia wananchi waliotembelea banda la shirika hilo kwenye banda kuu la Jakaya Kikwete.
 Wafanyaakzi wa Shirika la Posta Tanzania, wakiwahudumia wananchi waliotembelea banda la shirika hilo kwenye banda kuu la Jakaya Kikwete.
Bw. Kwiyukwa, (Kushoto), akifurahia jambo na Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano na elimu kwa umma, wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi. Sara Kibonde Msika, (kulia), na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Laura Kunenge.
Bw. Kwiyuka akipongezwa na Bi Laura Kunenge wa WCF, baada ya kutwaa tuzo hiyo

1 comment:

  1. Huduma za posta tangu mwanzoni zimechangia katika kuimarisha mawasiliano kati ya mataifa mengi na jamii mbali mbali.Ni muhimu kufahamu kuwa zawadi inatolewa tu kwa shirika ama mtu yule ambaye amefanya vizuri katika kazi yake. Hivyo basi, shirika la posta lina haki ya kuipokea zawadi hii.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.