Habari za Punde

Timu mpya ya madaktari kutoka nchini China yaanza kutoa huduma vijijini

 Wananchi wa Shehia ya Banko wakisubiri huduma za matibabu kutoka kwa timu ya madaktari bingwa kutoka China waliofika katika skuli ya sekondari Chumbuni kutoa hudua hizo.
 Daktari bingwa wa macho kutoka china Qin Qin akimfanyia uchunguzi wa macho mtoto Nassor Idrisa katika zoezi la kutoa huduma vijiji lililofanyika skuli ya sekondari Chumbuni.

 Mzee Abdalla Bakari akielezea matatizo ya afya yake kwa Dkt. He Qibin kutoka China wakati timu ya madaktari hao ilipokua ikitoa huduma za afya katika Shehiya ya Banko skuli ya sekondari Chumbuni (kulia) Dkt. Zulekha Bakari akisaidia tafsiri.

Dkt. Zhou Ziyue kutoka China akimpima sindikizo la damu (Pressure) Mzee. Ali Simai Makame wakati wa zoezi la kuchunguza afya wananchi wa Shehia ya Banko katika skuli ya sekondari Chumbuni.

Picha na Makame Mshenga.

1 comment:

  1. Shk Othman tunashkuru kwa kutupasha habari muhimu kama hizi. Nina ombi hebu tusaidie kujua lini watafika Pemba kutoa huduma za macho. Allah akufanyie wepesi katika kazi yako, Amiin.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.