Habari za Punde

Uzinduzi wa Maktaba ya Watoto Kisiwani Pemba.

Afisa Mipango na Sera Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Ramla Abass Farhan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maktaba ya Watoto, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya maktaba hiyo   iliyo mjini Chake chake Pemba.
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Madungu Chakechake Fatma Massoud na Hulaith Amour, wakisoma utenzi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maktaba ya Watoto Kisiwani Pemba katika eneo la Madungu Pemba.
WANAFUNZI wa Skuli za Madungu na Michakeni Msingi, wakisoma herufi za A B C hadi Z kwa kutumia Wimbo maalumu, wakati wa ufunguzi wa Maktaba ya Watoto Mjini Chake Chake
WANAFUNZI wa Skuli ya Madungu na Michakaeni msingi, wakionyesha umahiri wa kusoma hadithi kupitia Vitabu, wakati wa Ufunguzi wa Maktaba ya watoto mjini Chake Chake
WANAFUNZI wa Skuli za Madungu msingi na Michakeni wakionyesha umahiri wa kuimba wimbo na mchezo wakati wa ufunguzi wa Maktaba ya watoto mjini Chake Chake.
WANAFUNZI wa Skuli za Madungu msingi na Michakeni wakionyesha umahiri wa kuimba wimbo na mchezo wakati wa ufunguzi wa Maktaba ya watoto mjini Chake Chake.
AFISA mipango na sera kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Ramla Abass Farhan akizungumza na wafanyakaiz wa Maktaba kuu ya Pemba, wanafunzi na wazazi, wakati wa ufunguzi wa maktaba ya watoto Chake Chake Pemba.
MKUTUBI Mkuu wa Maktaba kuu ya Pemba, Mwacha Mohd Bakari akizungumza wakati wa ufunguzi wa maktaba ya watoto Mjini Chake Chake.


(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.