Habari za Punde

Waziri Haji Omar Khei azindua msimu wa uvunaji wa mpunga Msaani Pemba

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara maalumu, Haji Omar Kheir, akisalimiana na Wapiganaji wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) Kambi ya Msaani , kabla ya kuzinduwa uvunaji wa mpunga katika Kambi ya Msaani Pemba.
 Wapiganaji wa Jeshi la Kujenga Uchumi Pemba, wakishiriki katika uvunaji wa Mpunga uliolimwa na Wapiganaji hao , kabla ya kuzinduliwa uvunaji huo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Idara maalum huko Kisiwani Pemba.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikao , Serikali za Mitaa na Idara maalum, Haji Omar Kheir, akizinduwa uvunaji wa mpunga kwa msimu huu ambao umelimwa na Wapiganaji wa Jeshi hilo, huku akishirikiana na mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman, huko katika Kambi ya JKU Msaani -Pemba.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Idara maalumu za SMZ, Haji Omar Kheir, akizungumza na Wapiganaji wa Jeshi la Kujenga Uchumi Pemba, mara baada ya kuzinduwa Uvunaji wa mpunga kwa msimu huu huko katika Kambi ya Jeshi hilo Mssani Pemba.


Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar, Kanal Ali Mtumweni, akizungumza na Wapiganaji wa Jeshi hilo Kisiwani Pemba , mara baada ya uzinduzi wa uvunaji wa Kilimo cha mpunga katika Kambi za Msaani na kwa Pweza Pemba.


Picha na Said Abrahaman -JKU PEMBA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.