Habari za Punde

Zoezi la Uvunjaji wa Nyumba Kando ya Barabara ya Jangombe Lakamilika.

Zoezi la uvunjaji wa Nyumba kando ya barabara ya Jangombe limekamilika kwa wakaazi wa eneo hilo kumalizia kuvunja nyumba zao ili kuweza kupisha Mradi Mkubwa wa kupitishia maji machafu na ya mvua wakati wa mvua za masika zikinyesha baadhi ya maeneo hujaa maji na kuwa kero kwa wakazi hao na kuhama maeneo hayo baada ya kujaa maji.

Zoezi hilo limefanyika kwa kiasa kikubwa tayari eneo hilo husika likiwa wazi kusubiri hatua ya uchimbaji wa mtaro huo kuleta faraja kwa wananchi wa maeneo yanayojaa maji kupata usuluhishi wa kero hiyo baada ya ujenzi huo.  


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.