Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afanya Ziara Kutembelea Hospitali ya Wete na Kukabidhi Vifaa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akimsikiliza Daktari Dhamana wa Hospitali ya Wete Dr.Othman Maalim,wakati wa ziara yake kutembelea maendeleo ya Hospitali hiyo ya Wetu Pemba hutowa huduma za Afya kwa Wananchi wa Kisiwa cha Pemba kutoka maeneo mbalimbali hufika hospitalini hapo kupata matibabu bure. mara baada ya kutembelea chumba cha kuhifadhia dawa katika hospitali hiyo
WANANCHI mbali mbali wa Wilaya ya Wete, na Micheweni wakiwa katika eneo la hospitali hiyo kwa ajili ya kusubiri muda wa kuangalia wagonjwa wao wakati wa mchana, utaratibu wa kuangali wagonjwa katika hospitali huweka kwa vipindi vitatu asubuhi, mchana na jioni wananchi hupata fursa ya kuangaliwa wagonjwa wao. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seifa Ali Iddi, akimjulia hali mtoto wa kike aliyezaliwa leo katika Hospitali ya Wete, wakati alipofanya ziara ya kutembelea Wodi ya akina mama katika Hospitali hiyo
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akimzawadia mmoja ya watoto waliozaliwa leo katika Hospitali ya Wete, wakati alipotembelea chumba cha mama na watoto katika ziara yake ya Siku mbili Pemba
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seifa Ali Iddi, akizungumza na watendaji wa Wizara ya Afya Pemba, katika Hospitali ya Wete mara baada ya kufanya ziara katika hospitali hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi mashuka Daktari dhamana wa Hospitali ya Wete Othaman Maalim, ikiwa ni mchango wake kwa hospitali hiyo ya Wete
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi Geloni la Ditoli Daktari dhamana wa Hospitali ya Wete, Othman Maalim wakati alipoitembelea Hospitali hiyo
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe;Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi baskeli ya wagonjwa, Daktari dhamana wa Hospitali ya Wete, Othman Maalim mara baada ya kuitembelea hospitali hiyo na kuona changamoto zinazoikabili
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe;Balozi Seif Ali Iddi, akiitikia dua mara baada ya kumaliza kikao na watendaji wa Hospitali ya Wete, akiwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar
(Picha na Abdi Suleiman - PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.