Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Azindua Jukwaa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Dar es Salaam leo. 26/8/2017.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi la mkoa wa Dar es Salaam 

 :Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Jukwaa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi la mkoa wa Dar es Salaam.Na Mwandishi OMR.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewata wanawake wote washirikiane, wapendane na wasimame imara kuhakikisha nafasi ya mwanamke inaheshimika.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi mkoa wa Dar Es Salaam.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wanawake zaidi ya elfu tatu wa mkoa Dar Es Salaam, Mhe. Samia alisema Jukwa lililozinduliwa leo ni jukwaa la 23 la mkoa kufunguliwa.
Alisema mwakam 2015 dunia ilimaliza utekelezaji wa malengo 8 ya Milenia ambayo kulikuwa na lengo namba 3 linazungumzia usawa wa kijinsia kumwezesha mwanamke .
Alisema “Ni muhimu kuhakikisha kuwa ifikapo ukomo wa utekelezaji wa Ajenda ya Malengo Endelevu mwaka 2030,usawa wa mwanamke utakuwa umefikia asilimia 50 kwa 50 katika Nyanja zote ikiwemo ngazi ya maamuzi.”
Makamu wa Rais alisema lengo kubwa la kuanzisha majukwaa ya kumwezesha mwanamke kiuchumi nchini ni kuwaunganisha wanawake na fursa za masoko, mikopo ya riba nafuu na elimu ya ujasiriamali pia kubadilishana mawazo.

 Alisisitiza “Ni vyema pia kuhakikisha kuwa Majukwa haya yanakuwa na utaratibu wa kutembelewa ili kuweza kubadilishana uzoefu na pia fursa zikitokea zisambazwe kote hususani kwenye Majukwaa ya Vijijini ili kuhakikisha tunaenda mbele kwa pamoja. Miongoni mwetu humu kuna wabobezi wa masuala mengi; hivyo mnaweza kujipanga kubadilishana ‘experts’ na kuhakikisha kila Mwanamke Mtanzania ananufaika na keki ya Watanzania.”

Kaulimbiu ya uzinduzi wa jukwaa hilo ni “MWANAMKE TUMIA FURSA KUSHIRIKI UCHUMI WA VIWANDA”.  Wanawake wanaweza kujipanga na kuona namna gani wanaweza kujikomboa kiuchumi na kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika kujenga Tanzania mpya ya viwanda.  
Mhe. Samia alisema “Muda umefika sasa, wa kuwakomboa wanawake kutoka katika utumwa na lindi la umaskini linalotokana na kutowezeshwa kiuchumi, kuna umuhimu wa kuwapa ujuzi na maarifa; kuwawezesha kupata mikopo yenye riba nafuu na kwa urahisi; kukamilisha uanzishwaji wa programu ya utekelezaji ya kumwezesha mwanamke kupitia manunuzi ya umma; kuweka mifumo ya kisheria itakayopiga vita mila kandamizi; kuondoa vikwazo katika masoko; kuweka mifumo madhubuti ya kibenki na mifuko ya hifadhi za jamii hasa hifadhi ya Afya ili kujikwamua kwenye umaskini.
Mwishio Makamu wa Rais alihimiza katika kwa wanawake wengi kupata elimu ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwani kodi ni muhimu sana katika maendeleo ya Taifa.
Makamu wa Rais aliwashukuru Benki ya CRDB kwa kuchangia jukwaa hilo kwa kutoa hundi ya shilingi milioni 20 na pia aliwashukuru wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha mchakato wa kuunda jukwaa hilo unakamilika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.