Habari za Punde

Yaliojiri Wakati wa Hafla ya Harambee ya Kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Jumuiya ya UWT Zanzibar.

Picha ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein iliyochorwa ikipigwa mnada kwa Viongozi na Wafanyabiashara mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya Kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya UWT Zanzibar iliyofanyika jana katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitia saini Picha yake iliyochorwa ambayo ilipigwa mnada kwa Viongozi na Wafanyabiashara mbali mbali na kununuliwa kwa shingi za Kitanzania Milliomi tatu,ambayo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mecco Bw.Abdukadir Mohamed Bujet (kulia) ameinunua picha hiyo katika hafla ya Kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya UWT Zanzibar iliyofanyika jana katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akikabidhi Picha ya Mji wa Zanzibar Kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ikiwa ni miongoni mwa Picha mbali mbali zilizopigwa mnada kufanikisha kuchangia Mfuko wa maendeleo ya UWT Zanzibar hafla iliyofanyika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja,(kushoto) Mama Asha Suleiman Mke Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mecco Bw,Abdulkadir Mohammed  akimkabidhi picha Katibu wa UWT Taifa Mhe.Amina Makilagi aliyoinunua kwa njia ya mnada katika hafla ya Chakula cha jioni katika kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya UWT Zanzibar hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitia saini Picha yake ya kuchora iliyopigwa mnada na kuinunua Nd,Ali Kilupy wa Kendwa Rocky Hotel kwa thamani ya Silingi za kitanzania Millioni Mbili (katikati) wakati wa hafla ya Chakula cha jioni katika kuchangia Mfuko wa maendeleo ya UWT Zanzibar hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja,(kushoto) mjumbe wa kamati pia mwakilishi wa jimbo la Tunguu Simai Mohamed said
Katibu wa UWT Taifa Mhe.Amina Makilagi alipokuwa akipokea mchango kutoka kwa Akinamama mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya Chakula cha hisani cha kuchangia Mfuko wa maendeleo ya Wanawake Zanzibar katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiwahutubia wananchi na Viongozi wakati wa hafla ya Chakula cha jioni katika kuchangia Mfuko wa maendeleo ya UWT Zanzibar hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.