Habari za Punde

Mzrai Apania Kupandisha Daraja Timu Yake ya Kwerekwe City.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Baada ya kufanikiwa kupanda daraja la Pili Taifa msimu ulopita timu ya Kwerekwe City yenye Maskani yake Mwanakwerekwe Ijitimai imepania na msimu huu mpya kuondoka daraja hilo na kupanda daraja jengine.

Akizungumza na Mtandao huu katibu wa timu hiyo Mussa Habibu “Mzirai” amesema wamepania kupanda tena daraja kutoka la Pili Taifa hadi la kwanza na kutimiza malengo yao ya kucheza ligi kuu soka ya Zanzibar msimu wa mwaka 2019-2020.

Amesema falsafa yao ni umoja upendo na uwajibikaji hivyo haoni sababu ya kutopanda tena daraja kwani timu yake ina uongozi kamili na wachezaji wana ari kubwa sana.

“Baada ya kupanda daraja la pili taifa sasa akili yetu tumepania kucheza ligi daraja la kwanza taifa, tuna uongozi imara kama munavyowajua kina Mani Gamera au boss Moo, Bakari Rais, Ochu Gerrard na wengine wote hivyo hatuna sababu ya kupanda tena daraja na kutimiza ndoto zetu za kucheza ligi kuu msimu wa mwaka 2019-2020”. Alisema Mzirai.

Timu ya Kwerekwe City ilianzishwa mwaka 2014 ambapo msimu wa mwaka 2014-2015 ilicheza ligi daraja la tatu Wilaya ya Mjini na kufanikiwa kuwa Mabingwa ambapo msimu wa mwaka 2015-2016 walishiriki ligi daraja la pili Wilaya ya Mjini lakini hawakufanikiwa kupanda wakabakia apo apo na kupelekea msimu wa mwaka 2016-2017 kucheza tena daraja la Pili Wilaya ya Mjini na kufanikiwa kupanda daraja ambapo msimu mpya wa mwaka 2017-2018 watashiriki ligi daraja la Pili Taifa Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.