Habari za Punde

Oktoba 1 Kuaza Msimu Mpya wa Ligi Kuu ya Zanzibar Jumla ya Timu 28 Zitashiriki Huku Timu 12 Kushuka Daraja.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Msimu mpya wa ligi kuu soka ya Zanzibar wa mwaka 2017-2018 unatarajiwa kuanza Oktoba 1, 2017 ambapo timu 28 zitashiriki ligi hiyo kwa kila kanda timu 14, yani kanda ya Unguja 14 na Pemba 14.

Timu 4 za juu kila kanda zitashindana katika hatua ya 8 bora kutafuta nafasi yakuiwakilisha Zanzibar katika mashindano ya Kimataifa kombe la klabu bingwa na shirikisho barani Afrika ambapo timu 6 za mwisho kwa kila kanda zitashuka daraja huku timu 2 za juu kwa kila Kanda kutoka daraja la kwanza Taifa zitapanda ligi kuu na kufanya msimu wa mwaka 2018-2019 kuwa na jumla ya timu 20, yani kwa kila kanda kuwa na timu 10.

Kuhusu ligi daraja la kwanza taifa msimu wa mwaka 2017-2018 itajumuisha timu 16 ambapo ligi hiyo itachezwa kwa mfumo nyumbani na ugenini wakati huo huo timu 6 za chini zitashuka daraja nakucheza ligi daraja la pili taifa huku timu 2 za juu kutoka daraja la pili taifa zitapanda daraja la kwanza taifa.

Kuhusu ligi daraja la pili taifa ligi hiyo itakuwa na timu 36 ambapo ligi hiyo itachezwa kwa mfumo wa makundi ambapo zitapangwa kwenye makundi matatu na kila kundi kushuka timu 3.

“Ligi kuu tunatarajia kuanza Oktoba 1, 2017, baada ya kupokonywa uanachama kamili na CAF sasa msimu huu tutarejea tena kucheza vile vile ligi yetu kwa mfumo wa kanda yani Pemba na Unguja ambapo Pemba zitacheza timu 14 na Unguja 14 huku timu 6 za mwisho zikitarajiwa kushuka kila kanda na 4 za juu kucheza 8 bora”. Alisema Ali Bakar “Cheupe” ambae ni Afisa Habari wa ZFA.

Timu 28 zitakazocheza ligi kuu soka ya Zanzibar msimu mpya wa mwaka 2017-2018 ni JKU, Jang’ombe Boys, Zimamoto, Taifa ya Jang’ombe, Polisi, KMKM, Mafunzo, KVZ, Black Sailors, Chuoni, Kilimani City, Kipanga, Miembeni City na Charawe kwa upande wa Unguja na Pemba ni Jamhuri, Kizimbani, Mwenge, Okapi, Chipukizi, New Stars, Dogomoro, Wawi Star, Shaba, Young Islander, FSC, Hardrock, Chuo Basra na Opek.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.